Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Upelelezi kesi ya Wema Sepetu wakamilika

Thu, 14 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Februari 21, 2019 kumsomea maelezo ya awali mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu.

Hatua hiyo inatokana na upelelezi wa shauri hilo kukamilika na hivyo upande wa mashtaka kuiomba mahakama hiyo ipange tarehe kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo hayo.

Wema  anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika mitandaoni ya kijamii.

Leo Jumatano Februari 13, 2019 mwanasheria wa Serikali,  Glori Mwenda  ameieleza mahakama hiyo  mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonda  wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

"Shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na taarifa njema ni kwamba upelelezi wa shauri hili umekamilika, hivyo tunaomba tarehe  kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali, mshtakiwa huyu" amedai Mwenda.

Hakimu Kasonde baada ya kusikiliza maelezo hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 21, 2019.

Wema ambaye anatetewa na wakili, Ruben Simwanza, alifikishwa  kwa mara ya kwanza Kisutu Novemba Mosi, 2018 kujibu shtaka hilo. Wema yupo nje kwa dhamana.

Katika kesi ya msingi, Wema anadaiwa Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam alichapisha video ya ngono na kuisambaza katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

Soma Zaidi: Mahakama yahoji upelelezi kesi ya Wema kutokamilika



Chanzo: mwananchi.co.tz