Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Upelelezi dhidi ya Mdee, Bulaya na wenzao wakamilika

99157 Kina+mdee+pic VIDEO: Upelelezi dhidi ya Mdee, Bulaya na wenzao wakamilika

Mon, 16 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa upelelezi dhidi ya wafuasi 27 wa Chadema wakiwemo viongozi wawili ambao ni mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda mjini, Ester Bulaya wanaodaiwa kufanya fujo kutaka kuingia katika gereza  la mahabusu la Segerea umekamilika na jalada litatua kesho Jumatatu kwa mwanasheria wa Serikali. Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema Machi 13 mwaka huu saa 07:00 mchana jeshi hilo lilipokea taarifa kutoka kwa maofisa wa gereza hilo kuwa kuna kundi la wafuasi wa Chadema limekusanyika katika geti la kuingilia gerezani hapo huku likiandamana na kufanya fujo. Amesema wafuasi hao walifanya vurugu hizo walipokuwa wakienda kumtoa mwenyekiti wao Freeman Mbowe ambapo walikwenda kufanya vurugu kutaka kumtoa kabla ya kukamilisha taratibu. “Tulifika eneo la tukio na kukuta askari wa magereza wakiendelea kuwadhibiti wanachama hao ndipo polisi walipowakamata watuhumiwa 27 na kuwapeleka katika kituo cha polisi Stakishari kwa mahojiano,” amesema. “Baada ya mahojiano watuhumiwa wote 27 walidhaminiwa kwa mujibu wa sheria na watafikishwa mahakamani hivi karibuni kwani upelelezi wa shauri hili umeshakamilika,” ameongeza. Hata hivyo, Kamanda Mambosasa alitumia mkutano huo kutoa rai kwa kikundi chochote cha siasa, dini, au mtu yeyote kuacha kuchezea maeneo nyeti kama vile magereza, makambi ya majeshi yote au maeneo yoyote ambayo ni nyeti kwa kwa Taifa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu au kikundi chochote kitakachokiuka taratibu na sheria zilizowekwa. “Kwa hiyo niwaombe wananchi wote ndani ya kanda kuheshimu taratibu za nchi na kufuata miongozo yote inayotuweka salama kinyume na hapo mnatuita sisi tufanye kazi yetu magereza ni eneo ambalo linatunza wafungwa ambao wapo kisheria hivyo ni eneo ambalo linapaswa kuheshimiwa,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz