Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Ukweli lilipo jalada kesi ya ofisa wa LHRC huu hapa

VIDEO: Ukweli lilipo jalada kesi ya ofisa wa LHRC huu hapa

Wed, 4 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili ofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHCR), Tito Magoti na mwenzake umeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hawajui kinachofanyika kwa kuwa jalada la kesi hiyo liko polisi.

Februari 19, 2020 Mahakama hiyo iliutaka upande wa mashtaka kueleza upelelezi washauri hilo umefikia wapi ili kujua kama  unakwenda mbele au umesimama.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani Desemba 24, 2019 wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kumiliki programu ya kompyuta iliyotengenezwa mahsusi kufanya kosa la jinai na kuwawezesha kujipatia Sh17.3 milioni.

Wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo  Saimon amedai hayo leo Jumatano Machi 4, 2020 mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo, Janeth Mtega wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Amedai hawajui  kwa sasa kinachofanyika,  polisi watakapomaliza upelelezi jalada  wataliwasilisha ofisi ya mwendesha mashtaka.

"Tarehe iliyopita Mahakama ilituelekeza kueleza upelelezi ulipofikia, jalada bado liko polisi na wanaendelea na upelelezi hautujui kinachofanyika tunasubiri watakapomaliza wataliwasilisha ofisi ya mwendesha mashtaka,” amedai Wankyo

Pia Soma

Advertisement

Wakili wa utetezi,  Fulgence Masawe amedai kama jalada liko polisi ni jukumu lao kushirikiana na mwendesha mashtaka kuhakikisha upelelezi unakamilika na kesi hiyo inaanza  inasikilizwa.

"Shida yetu ni kuona haki inatendeka  makosa walioshtakiwa nayo hayana dhamana, washtakiwa wako ndani hawana tofauti na wanaotimikia kifungo," amedai wakili Masawe.

 

Hakimu Mtega amesisitiza kuharakishwa kwa upelelezi huku akiahirisha kesi hiyo hadi Machi 18, 2020.

 

Mashtaka mengine yanayowakabili ni  kumiliki programu ya kompyuta iliyotengenezwa mahsusi kwa ajili ya kutenda makosa ya jinai na kujipatia Sh17.3 milioni wakijua mapato hayo yametokana na mazalia ya kosa la kushiriki genge la uhalifu.

Chanzo: mwananchi.co.tz