Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Serikali yaahidi kumrudisha kwa nguvu Magreth Gonzaga

Video Archive
Thu, 28 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali imeagiza mtuhumiwa wa utakatishaji fedha Magreth Kobelo Gonzaga anayedaiwa kutorokea nje ya nchi ajisalimishe haraka iwezekanavyo kabla haijachukua hatua za kisheria kumrudisha nchini kwa nguvu.

Agizo hilo limetolewa ikiwa ni siku moja tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kumtaka ajisalimishe haraka ili kujibu tuhuma za kujihusisha na utakatishaji wa fedha haramu kabla mali zake hazijataifishwa.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumatano Machi 27, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuna sheria za kimataifa na za nchini kwa nchi kushirikiana na kurejesha watu ambao wanakabiliwa na mashtaka katika nchi moja na wakawa wamekimbilia katika nchi nyingine.

“Wanaweza kuwa ni raia wa nchi nyingine au hata raia wa Tanzania, kwa mfano hapa Tanzania tumekwishapokea maombi kutoka nchi zingine kuwarejesha wahalifu ama Watanzania ambao walikuwa wanaishi huko wamefanya makosa, kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa niseme wazi hayuko salama kwa sababu jumuiya yote inashirikiana kupambana na uhalifu,” amesema Profesa Kabudi.

Kauli hiyo ya Profesa Kabudi imekuja siku moja baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna Diwani Athuman kusema walitoa tangazo la kutafutwa kwa Magreth katika vyombo vya habari na majukwaa mbalimbali ikiwamo gazeti la Mwananchi akituhumiwa kutakatisha fedha.

Alisema Magreth ni mkazi wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambaye anatuhumiwa kutakatisha fedha na kujipatia mali kupitia moja ya kampuni aliyokuwa akifanya kazi.

Related Content

Diwani alisema wakati uchunguzi ukiendelea, Magreth alitoweka.



Chanzo: mwananchi.co.tz