Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Polisi Arusha yakamata 13 kwa tuhuma za uhalifu

Video Archive
Sat, 7 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Polisi Mkoa wa Arusha nchini Tanzania linawashirikia watu 13 wa kwa madai ya wizi wa  samani mbalimbali na kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 6, 2019 Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Jonathani Shana amesema watuhumiwa hao walikamatwa kwa siku tatu maeneo ya Sanawari Kata ya Moivo wilaya Arusha mjini .

Kamanda Shana amesema vitu vilivyokamatwa ni  jokofu, radio, kompyuta, pikipiki nne, meza, pamoja na madawa ya kulevya aina ya bangi, heroin na mirungi.

"Baadhi ya vitu walivyotuonyesha ndio tulivyovileta hapa hivyo niwaombe wananchi waje kutambua vitu vyao kwa vithibitisho ikiwemo pikipiki nne aina kinglion zenye namba za us MC504AHT,"amesema

Kamanda Shana amesema kuna pikipiki tatu aina ya boxer MC262AXQ na MC240AGB na MC811BWG pamoja na kuziiba walizitumia katika usafiri wa uporaji maarufu Kama tatu mzuka.

Shana amesema wenye pikipiki hizo na vitu vingine kama  hawatajitokeza zitataifishwa kuwa za serikali.

Pia Soma

Advertisement
"Bado tunaendeleza vita dhidi ya madawa ya kulevya ikiwa wanaojihusisha na dawa hizo ni heri waache wafanye shughuli nyingine kwani hatutalala wala kukaa hadi Arusha itakapokuwa shwari," amesema

Amesema katika msako huo , wamefanikiwa kukamata bangi kilo 12, rumbesa 16 za mirungi pamoja na kete mbili za heroin.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz