Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Naibu waziri atoa maagizo kwa polisi juu ya kifo cha mwanafunzi wa KIU

Video Archive
Wed, 19 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi nchini Tanzania, Hamad Masauni amesema Jeshi la Polisi tayari limewatambua watu waliohusika katika tukio la shambulio lililo sababisha kifo cha Anifa Mgaya.

Anifa (21) ambaye alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Stashahada katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) tawi la Tanzania, alifikwa na umauti usiku wa juzi Jumapili Juni 16, 2019 nje ya geti la chuo hicho baada ya kuchomwa na vitu vyenye nchi kali na watu wanaodhaniwa ni vibaka.

Masauni ametoa kauli hiyo leo Jumanne Juni 18, 2019 nyumbani kwa akina Anifa, Salasala Dar es Salaam wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo kabla ya kusafirishwa kwenda Makambako mkoani Iringa kwa maziko.

Naibu waziri huyo amewaagiza pia makamanda wote wa wilaya za Dar es Salaam waliokuwepo msibani hapo, kuwachukulia hatua kali wahusika wote ili iwe fundisho kwa wengine.

Amesema jeshi la polisi limelichukulia tukio hilo kwa uzito na linawahakikishia wanafunzi wa vyuo vyote vikuu vyote, wataboresha usalama wao ili matukio kama hayo yasiendelee kutokea.

“Ndani ya muda mfupi naamini watuhumiwa hao waliotambuliwa watashughulikiwa na majibu kutolewa kwa sababu tunataka kuhakikisha wanafunzi wetu wanasoma kwa amani, Mkoa wa Dar es Salaam kitakwimu ndiyo unaoongoza kwa matukio ya uhalifu, lakini tutahakikisha tunatokomeza megenge yote ya kihalifu nchini.

Habari zinazohusiana na hii

“Binti huyu hana hatia alikuwa anajisomea na ana ndoto kubwa. Taifa lilikuwa likimtegemea aweze kutoa mchango wake katika siku za baadaye lakini wahalifu wachache wamekatisha ndoto za binti huyu,” amesema Masauni.

Amesema wahalifu wanaotegemea kazi hiyo kujipatia kipato ni bora watafute shughuli nyingine za kufanya kabla ya kutiwa mbaroni.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambo sasa amesema suala hilo hawataliacha lipite, bali watahakikisha wahusika wanajutia tukio hilo.

“Jumuiya ya wanafunzi wa KIU nimeyasikia maoni yenu na mengine mliyokuwa mkiyaandika katika chuo kikuu cha Dar es Salaam tutayafanyia kazi ndani ya muda mfupi na matukio haya hatutaki yatokee katika vyuo vyetu kwa sababu ni kichefuchefu na kifo chochote kinauma,” amesema

Chanzo: mwananchi.co.tz