Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mwanamke shujaa aliyepambana na Majambazi Kigoma"Jambazi Nikamkamata'

Video Archive
Wed, 12 Jan 2022 Chanzo: millardayo.com

Usiku wa January 10, 2022 baada ya Mtu mmoja ambaye hajafahamika jina mwenye umri unaokadiriwa kua miaka 30 -40 kuuawa kwa kujeruhiwa na risasi akiwa anatekeleza tukio la Ujambazi wa kutumia silaha katika mtaa wa mrusi Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma  ACP James Manyama amesema Majambazi watatu akiwemo Marehemu walivamia nyumbani kwa Castor Benard na kumpora Pikipiki na kumjeruhi paja la miguu wa kushoto ndipo kikosi cha  Jeshi la Polisi kufika eneo la tukio wakishirikiana na Wananchi  walifika eneo la tukio na kumjeruhi jambazi mmoja  wakati wakirushiana na risasi na Jambazı huyo kufariki.

Hapa nakukutanisha na Mke wa Castor Benard aliyapambana na Jambazi usiku wa tarehe 10 na kuonyesha ujasiri wa hali ya juu ambapo mkuu wa Wilaya ya Kasulu kanal Issac Mwakisu na Kamanda wa Polisi wa Kigoma walimpongeza mwanamke huyo kwa kuonyesçha ujasiri wa hali ya juu kupambana na majambazi hao.

Chanzo: millardayo.com