Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Muuguzi adaiwa kubaka mjamzito wakati akijifungua

89335 Abakwapic VIDEO: Muuguzi adaiwa kubaka mjamzito wakati akijifungua

Fri, 20 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Katavi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia ofisa muuguzi msaidizi wa kituo cha afya Mamba Wilaya ya Mlele, Abednego Nkona (32) kwa tuhuma za kumbaka mjamzito wakati akijifungua.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Katavi, Benjamin Kuzaga alisema tukio hilo limetokea juzi saa 2.00 usiku.

Alisema mjamzito huyo alifika katika kituo hicho cha afya kwa ajili ya kujifungua na wakati mtuhumiwa akimpima njia, alimbaka.

“Mwanamke huyo alihisi hali isiyokuwa ya kawaida sehemu zake za siri, alishtuka na kumuona mtuhumiwa amemuingilia kimwili.

“Baada ya kufanyiwa kitendo hicho, mjamzito alinyanyuka kitandani na kwenda kutoa taarifa kwa mzazi mwenzake wake Mektrida Deogratius mkazi wa Majimoto,” alisema.

Polisi mkoani Katavi wanatarajia kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo wakati wowote ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Akizungumza na Mwananchi Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rachel Kasanda alisema, “huyu mwanamke hana hali mbaya, alikuwa hajaumwa uchungu sana na alikuwa akitembea mwenyewe, pia tunafuatilia ukaribu wao na mtuhumiwa.”

“Bado yupo kituo cha afya, mtuhumiwa aliwekwa chini ya ulinzi na mwanamke huyo alihojiwa pamoja na wagonjwa wengine na mama yake mzazi ili kujua waliona au kusikia nini. Mjamzito huyo pia alikwenda kupimwa.”

Chanzo: mwananchi.co.tz