Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mama wa bilionea Msuya atoa sababu za kutofuta kesi

VIDEO: Mama wa bilionea Msuya atoa sababu za kutofuta kesi

Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. NdeshukurwaSikawa ambaye ni mama mzazi wa marehemu bilionea, Erasto Msuya amegoma kufuta kesi ya kugombea mali za mwanae.

Ndeshukurwa katika kesi hiyo ambayo leo Ijumaa Novemba 29, 2019 imetajwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha anataka Mahakama kumuondoa mjane wa bilionea Msuya, Miriam Mrita kuendelea kuwa msimamizi wa mirathi akimtuhumu kuuza mali bila utaratibu.

Hata hivyo, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Yohane Masara hakuwepo mahakamani na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Julius Nkwabi akaahirisha kesi hiyo hadi Desemba 13, 2019 ambapo hukumu ya mapingamizi itatolewa.

Miriam kupitia wakili wake, Shilinde Ngalula ameweka pingamizi juu ya shauri hilo, kwa hoja kuwa tayari limetupwa mara mbili na Mahakama Kuu kutokana na shauri hilo la mirathi tayari lilifungwa.

Awali, Naibu MsajiliĀ  Nkwabi amemtaka wakili wa mama wa bilionea huyo, Fadhili Nangawe kupeleka barua mahakamani kama wanataka kesi hiyo kusimama kupisha mazungumzo ya familia.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu, Ndeshukurwa amesema hakusudii kuifuta kesi hiyo kwani hajui kitatokea nini kama mashauriano yaliyoitishwa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro yatakwama.

"Ambacho tunaweza kuomba kesi kusogezwa mbele ili kupisha mashauriano ambayo tulikubaliana na sio kuifuta kesi hii," amesema

Bilionea Msuya aliuawa Agosti 7, 2019 wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kwa kupigwa risasi akiwa katika biashara ya kuuziana madini na baadaye mke wake, Miriam Mrita alikamatwa kwa tuhuma za mauwaji ya mdogo wa bilionea huyo, Aneth Msuya na kesi yake inaendelea jijini Dar es Salaam.

Chanzo: mwananchi.co.tz