Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mahakama yawakuta na hatia Malkia wa Tembo, wenzake

Video Archive
Tue, 19 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewatia hatiani washtakiwa watatu akiwemo raia wa China,  Yang Feng Glan (66) waliokuwa wanakabiliwa na  mashtaka ya kufanya biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh 13bilioni.

Mbali na Glan, maarufu kama Malkia wa Tembo, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Salvius Matembo na Philemon Manase.

Akizungumza leo Jumanne Februari 19, 2019, hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Huruma Shaidi amesema amewatia hatiani  washtakiwa hao.

Hata hivyo, mahakama hiyo, itatoa adhabu  leo saa tano asubuhi hii  na kesi imeahirishwa kwa muda.

VIDEO: Hukumu kesi ya Malkia wa Tembo Februari 19





Chanzo: mwananchi.co.tz