Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mahakama yamhukumu mchungaji na wake zake kwenda jela, kulipa faini

Video Archive
Tue, 10 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam nchini Tanzania imemuhukumu Mchungaji wa Kanisa la The Early Church of Lord Yeshwah, David Chirhuza (33) kulipa faini ya Sh2 milioni au kutumikia kifungo cha miaka miwili.

Wakati huohuo, mahakama hiyo imewahukumu Eather Sebuyange (27), Kendewa Ruth (26) ambao ni wake wa mchungaji huyo na Samwel Samy (22) kulipa faini ya Sh1 milioni au kwenda jela mwaka mmoja kila mmoja.

Akitoa Hukumu hiyo leo Jumanne Septemba 10, 2019 Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando amesema baada ya kulipa faini au kutumikia kifungo hicho watuhumiwa hao wanatakiwa kurudishwa nchini kwao.

Katika shtaka la kwanza mchungaji huyo na wenzake ambao ni raia wa Kongo walibainika kuishi nchini Tanzania bila kibali ambapo wamehukumiwa kulipa faini ya Sh1 milioni kila mmoja au kwenda jela mwaka mmoja kila mmoja.

Katika shtaka la pili, linalomkabili Chirhuza ambaye ni mchungaji raia wa Kongo na mchungaji wa kanisa hilo  alikutwa akifanya kazi ya kiuchungaji bila ya kuwa na leseni na leseni ya ukazi hivyo amehukumiwa kulipa faini ya Sh1 milioni kila mmoja au kwenda jela mwaka mmoja kila mmoja.

 

Pia Soma

Advertisement
Endelea kufuatilia Mwananchi wa habari zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz