Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Hukumu kesi ya mirathi ya Bilionea Msuya kutolewa Desemba 13

VIDEO: Hukumu kesi ya mirathi ya Bilionea Msuya kutolewa Desemba 13

Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Desemba 13 mwaka huu inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya kugombea usimamizi wa mirathi ya mali za marehemu bilionea Erasto Msuya.

Kesi hiyo imefunguliwa na mama mzazi wa bilionea huyo, Ndeshikurwa Sikawa ambaye amegoma kufuta kesi hiyo.

Usikilizwaji wa kesi hiyo umekuwa ukivuta umati wa wasikilizaji mbele ya Jaji wa Mahakama kuu Kanda ya Arusha, Yohane Masara ambamo Ndeshikurwa amefugua kutaka, mjane wa mahehemu Msuya, Miriam Mrita kuondolewa kuwa msimamizi wa mirathi hiyo akimtuhumu kuanza kuuza mali za marehemu mume wake.

Miriam kupitia wakili wake, Shilinde Ngalula aliweka pingamizi juu ya shauri hilo, kwa hoja kuwa tayari limetupwa mara mbili na Mahakama Kuu kutokana na shauri hilo kuwa tayari lilifungwa.

Hata hivyo, uamuzi juu ya shauri hilo ulipangwa kutolewa jana hata hivyo, Jaji Masara hakuwepo hivyo naibu msajili wa Mahakama Kuu, Julius Nkwabi aliahirisha hadi Desemba 13 kwa ajili ya uamuzi.

Wakili Fadhili Nangawe anayemtetea mama wa bilionea huyo aliomba kabla ya hukumu hiyo kutolewa mteja wake aliomba shauri hilo kusitishwa ili wafanye mazungumzo nje ya mahakama.

Hata hivyo, Nkwabi alimtaka wakili huyo ambaye tayari alikwishajibu mapingamizi kuandika maombi hayo kwa barua maalum kabla ya hukumu, kwani tayari Jaji alikwishajiandaa kuandika hukumu huyo ambayo itatolewa Desemba 13.

SOMA ZAIDI

Chanzo: mwananchi.co.tz