Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Hukumu kesi ya kina Mbowe saa saba, ulinzi waimarishwa

Video Archive
Tue, 10 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Wakati hukumu ya kesi inayowakabili viongozi wanane wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ikitarajiwa kusomwa saa saa saba mchana jeshi la polisi limeimarisha ulinzi.

Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Dk Vicent Mashinji ambaye ni katibu mkuu wa zamani wa Chadema. Dk Mashinji alihamia CCM Februari 18, 2020.

Katika kesi hiyo namba 112 ya mwaka 2018 washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kati ya Februari 1 na 16, 2018.

Awali kesi hiyo ilipangwa kusomwa saa 4:30 wakati washtakiwa wakiwa ndani ya ukumbi, walifahamishwa kupitia kwa Wakili wao Peter Kibatala kuwa muda umesogezwa hadi saa 7:30 mchana.



Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Viongozi mbalimbali wa Chadema wakiwemo wabunge na wenyeviti wa kanda ni miongoni mwa watu waliojitokeza kusikiliza hukumu hiyo.

Wengine ni kutoka vyama vingine vya upinzani akiwemo Mshauri wa ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad.

Pamoja na ulinzi kuimarishwa baadhi ya wanachma na viongozi hao wamekaa vikundi wakijadiliana mambo mbalimbali.

Mbali na Mbowe na Dk Mashinji, washtakiwa wengine ni katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika; naibu katibu mkuu Salum Mwalimu (Zanzibar) na mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Pia wamo mbunge wa Tarime mjini, Esther Matiko; mbunge wa Kawe, Halima Mdee; mbunge wa Bunda, Esther Bulaya; mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Chanzo: mwananchi.co.tz