Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Familia ya kigogo wizara ya fedha anayedaiwa kuuawa yasema kifo cha ndugu yao si cha kawaida

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Familia ya aliyekuwa Ofisa Mwandamizi Wizara ya Fedha na Mipango, Leopold Lwajabe imesema kifo cha ndugu yao kinaonyesha hakikuwa cha kawaida.

Lwajabe aliyekuwa mkurugenzi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini (EU) kupitia wizara hiyo, mwili wake ulikutwa wilayani Mkuranga mkoani Pwani Julai 26, 2019 ukining’inia juu ya mti wa mwembe kwa mujibu wa familia yake.

Akizungumza na Mwananchi jana jioni Jumanne Julai 30, 2019 nyumbani kwa marehemu Tabata Kinyerezi, msemaji wa familia, Mugisha Brassio alisema kwa namna mwili ulivyokutwa inaonyesha wazi alipata mateso kabla ya kifo chake.

“Kinachotushangaza alivyotoweka mara ya pili aliondoka akiwa amevaa suruali nyeusi, viatu vyeusi na shati jeupe la mistari, lakini jana (juzi) tulipoonyeshwa mwili kwa ajili ya utambuzi alikuwa amevaa suruali na viatu vilevile ila alivaa fulana ya bluu yenye mistari mieupe ambayo ni nguo mpya hakuwahi kuwa nayo,” alidai ndugu huyo.

Akielezea kupotea mara ya kwanza, alisema Lwajabe alitoweka Julai 16, 2019 akiwa ofisini, alipigiwa simu na mtu ambaye alifika ofisini hapo kwa mazungumzo. Wanadai tangu hapo walimtafuta bila mafanikio hadi aliporejea Julai 19 saa 12:30 asubuhi.

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Jumatano Julai 31, 2019.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz