Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Familia ya 'Mo Dewji': Tunamshukuru Rais Magufuli

Video Archive
Sat, 20 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Familia ya mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohamed Dewji 'Mo' imemshukuru Rais John Magufuli jinsi alivyofanikisha kupatikana kwa bilionea huyo kijana Afrika.

Msemaji wa familia, Azzim Dewji akizungumza nyumbani kwa 'Mo' leo asubuhi Jumamosi Oktoba 20, 2018 amesema,"Tumempaka na tunamshukuru Mungu."

Amesema afya ya 'Mo' aliyetekwa alfajiri ya Alhamisi wiki iliyopita Oktoba 11,2018 jijini Dar es Salaam, Tanzania 'ni nzuri asilimia 100' sema labda sababu alitekwa inaweza kuwa tatizo kisaikolojia.

Azzim amesema,"Amepatikana mida ya saa 8.30 usiku, walimuacha halafu yeye (Mo) akapiga simu kwa baba yake."

"Tunamshukuru sana Rais (John Magufuli) kwa kuagiza vyombo vyake vya usalama na vyombo vyake tumempata," amesema Azzim

Msemaji huyo amesema baadaye kutakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaomhusisha 'Mo' Dewji.

Endelea kufuatilia MwananchiBilionea 'Mo' Dewji apatikana

Polisi Tanzania wabaini gari lililomteka Mo Dewji

Kauli ya Sirro kuhusu utekwaji wa Mo Dewji yazua mjadala mtandaoni

Endelea kufuatilia Mwananchi

 

Chanzo: mwananchi.co.tz