Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: DPP aridhia maombi ya Kabendera kukiri mashtaka

VIDEO: DPP aridhia maombi ya Kabendera kukiri mashtaka

Wed, 26 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania nchini Tanzania (DPP) ameridhia maombi ya mwandishi wa habari, Erick Kabendera  aliyoyawasilisha kwake akiomba kukiri mashtaka yanayomkabili na kuomba msamaha.

Mbali na kuridhia maombi hayo, DPP amewasilisha hati ya kuiruhusu Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Kabendera.

Maelezo hayo yametolewa leo Jumatatu Februari 24, 2020 na wakili wa Serikali mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiana na wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon

Nchimbi ameieleza Mahakamani  hiyo mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Janeth Mtega.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kutakatisha Sh 173milioni.

Kabendera alimuandikia  barua DPP akiomba asamehewe na apunguziwe adhabu.

Pia Soma

Advertisement
Hata hivyo,  mahakama  imepokea kibali hicho na kuruhusu upande wa mashtaka kumsomea mashtaka yake.

Kabendera ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea wa ndani na nje alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu.

Mashtaka hayo ni kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya Sh173.2 milioni.

Kesi bado inaendelea.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz