Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utetezi wataka kuharakishwa kesi wafanyakazi wa NIC

HUKUMU Utetezi wataka kuharakishwa kesi wafanyakazi wa NIC

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upande wa utetezi katika kesi inayowakabili waliokuwa watumishi saba wa Shirika la Bima la Taifa akiwemo Mhasibu Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa, Tabu Kingu wameutaka upande wa mashtaka kuharakisha kuandaa taarifa kwa ajili ya kupeleka Mahakama Kuu.

Washtakiwa hao wanakabiliwa mashitaka 365 likiwemo la utakatishaji fedha na kuisababishia shirika hilo hasara ya zaidi ya Sh1.8 bilioni.

Wakili wa utetezi, Hekima Mwasipo aliieleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Evodia Kyaruzi alidai kwa zaidi ya mwezi mmoja upande wa mashtaka wanapokuja mahakamani hapo wamekuwa wakieleza kuwa wanaandaa taarifa kwa ajili ya kupeleka Mahakama Kuu.

"Upande wa mashtaka mharakishe kuandaa hiyo taarifa kwa ajili ya kupeleka mahakama kuu na wanatakiwa kujua washtakiwa hawa wanahitaji kupata haki yao ya msingi kwa kuwa wapo mahabusu wanazidi kuumia,”amedai Mwasipo.

Awali Wakili wa Serikali, Monica Ndakidemi alidai kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa upelelezi umekamilika wanaandaa taarifa kwa ajili ya kupeleka Mahakama Kuu.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Agosti 28, 2023 kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Kingu washtakiwa wengine ni

Peter Nzunda mhasibu, Samwel Kamanga, Victor Mleleu, Kenan Mpalanguro, Lusuboro Sambo na Mafworo Ngereja.

Katika kesi ya msingi kati ya Januari Mosi, 2013 hadi Desemba 31,2018, katika maeneo tofauti Mkoa wa Dar es Salaam, Rukwa, Kilimanjaro, Morogoro, Mbeya, Arusha na Kigoma washtakiwa hao walilisababishia shirika hilo hasara ya zaidi ya Sh8 bilioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live