Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uteketezaji vielelezo kesi ya mauaji mwanafunzi Scolastica wakwama

65384 Pic+svcolatica

Thu, 4 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Zoezi la kuteketeza vielelezo vilivyotumika kama ushahidi katika kesi ya mauaji ya mwanafunzi wa shule ya Scolastica, Humphrey Makundi(16) imegonga mwamba  baada ya mawakili wa utetezi kutaka wateja wao kuwepo.

Wakati akitoa hukumu ya kesi hiyo Juni 3, 2019, Jaji wa Mahakama Kuu, Firmin Matogolo aliagiza vielelezo hivyo, panga lililotumika katika mauaji hayo na nguo za marehemu kuteketezwa.

Vielelezo vingine vilikuwa ni simu za washtakiwa walizotumia kuwasiliana usiku na kuitana eneo la tukio, ambazo jaji huyo aliamuru zitaifishwe na Serikali.

Awali, akiwasilisha ombi la kusitisha kazi hiyo mbele ya naibu msajili wa mahakama hiyo, wakili Elikunda Kipoko ameeleza umuhimu wa wateja wake kuwepo, kwamba baadhi yao wameshakata rufaa.

"Suala la kuchoma vielelezo hivi haliwezi kufanyika bila wateja wetu kuwepo, hapa inatakiwa umakini kwa sababu zoezi ili lifanyike lazima wateja wetu wawepo,” amedai wakili Kipoko.

Hata hivyo,  wakili wa Serikali Lucy Kyusa aliyekuwa akisikiliza kesi  hiyo alieleza kuwa  zoezi hilo lipo kisheria kutokana na amri  iliyotolewa na mahakama.

Pia Soma

Naibu msajili wa mahakama hiyo, Frank Mahimbari ameeleza kuwa kutokana na kuwa washtakiwa wote hawapo mahakamani, ataandika samansi ili waletwe mahakamani kushuhudia zoezi hilo.

June 3, 2019 mahakama hiyo ilimhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa mlinzi wa shule hiyo, Hamis Chacha ,huku mmiliki wa shule hiyo, Edward Shayo pamoja na aliyekuwa mwalimu wa nidhamu, Laban Nabiswa wakihukumiwa kifungo cha miaka minne jela kila mmoja kwa kuficha ukweli wa mauaji ya mwanafunzi  huyo.

Novemba 6, 2017 mwanafunzi huyo aliuawa na kisha mwili wake kutupwa katika mto Ghona mita 300 kutoka ilipo shule hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz