Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utata vifo vya vijana watatu

MAITI YAPOTEA Utata vifo vya vijana watatu

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Utata umeghubika vifo vya vijana watatu wanaotuhumiwa kwa uhalifu, ambao ndugu wa marehemu wanadai walichukuliwa na polisi wilayani Temeke na miili yao ikakutwa baadaye hospitalini.

Vifo hivyo vimetokea wakati polisi mkoani Mara wakilalamikiwa pia kuua watu watatu wilayani Serengeti waliodaiwa kuwa wahalifu, katika mazingira yanayofanana.

Katika matukio hayo mawili, familia za marehemu zimelalamika kuwa waliouawa hawakukutwa kwenye maeneo ya uhalifu, bali walichukuliwa nyumbani.

Tukio hilo limetokea zikiwa zimepita wiki mbili tangu Jeshi la Polisi Kanda Maalumu litangaze kuua watu sita, waliotajwa kuwa walikuwa wanakwenda kutekeleza tukio la kihalifu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke Richard Ngole alipoulizwa kuhusu madai hayo alisema, suala hilo atafutwe Kamanda wa Polisi Kanda Maalum.

Kamanda wa Kanda Maalum Jumanne Muliro alipotafutwa hakutaka kuzungumzia vifa hivyo, bali alisema wananchi kwenye mtaa huo wamekuwa wakilalamikia baadhi ya vijana kujihusisha na vitendo vya kihalifu ikiwemo uporaji na kufikia hatua ya kutaka kuchoma moto nyumba za wazazi wa vijana hao.

“Hiyo taarifa naendelea kuifuatilia nitaitolea taarifa, baadaye huo mtaa unaouzungumziwa wananchi wamekuwa wakiandamana kutaka kuchoma nyumba za wazazi wao, hatuwezi kuacha fujo ziendelee,” alisema Muliro.

Muliro aliongeza kuwa jeshi hilo limekuwa linalalamikiwa na wananchi kwa kuwaachia wahalifu ambao hurudi katika maeneo yao kuendelea na uhalifu.

“Maeneo mengi wananchi wamechoka hadi kufikia wakati wanataka kuwachoma moto, lakini sisi tunafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi na mali zao wanakuwa salama.”

Akizungumza juzi kwenye mjadala uliofanyika kwa njia ya mtandao, Kamanda Muliro amesema jeshi hilo hulazimika kutumia nguvu iwapo mazingira yanachochea hilo kutokea.

“Kila mtu ana haki ya kuishi ila inapotokea mmoja anataka kusababisha mwenzake awe kwenye mazingira ya hatari ya kutokuishi, pale ile nguvu inayotumika inahesabiwa kama nguvu ya kadri,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live