Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utata anayedaiwa kujinyonga kwa wivu wa mapenzi

77314 Ajinyongapic

Thu, 26 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Buchosa. Mashaka  Zakaria (26), mkazi wa wilayani Sengerema  Mkoa wa Mwanza amejinyonga hadi kufa huku rafiki yake akidai alichukua uamuzi huo baada ya kumkuta mpenzi wake akicheza muziki na mwanaume mwingine.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia  jana Jumatano Septemba 25, 2019 katika kijiji  cha Bukokwa kata ya Bukokwa.

Juma Italazo, rafiki wa Zakaria amesema mwili wake ulikutwa ukining’inia katika mti wa mwembe ulipo kando ya barabara saa kadhaa baada ya kutokea hali ya kutoelewana na mpenzi wake aliyemkuta akicheza muziki disko.

Mkuu wa polisi Wilaya ya Sengerema, Maili Makoli amesema wanaendelea na uchunguzi na atakayebainika kuhusika na kifo hicho atachukuliwa hatua.

Asteria Gerevazi (23), mke za Zakaria amesema mumewe alimuaga usiku baada ya kumaliza kula chakula kuwa anakwenda disko lakini hakurejea hadi asubuhi alipoelezwa kuwa mwili wake umekutwa katika mti huo.

“Hatukuwa na ugomvi wowote na mume wangu nashangazwa na jambo lililotokea,” amesema  Anastazia.

Pia Soma

Advertisement
Katika maelezo yake, Italazo amesema baada ya Zakaria kumshuhudia mpenzi wake akisakata muziki na mwanaume mwingine alikasirika na kuibuka mvutano kati yao.

“Baada ya hapo aliniambia anakwenda nyumbani lakini niliposikia amejinyonga nikajua wazi kisa kilikuwa hicho,” amesema Italazo.

Ofisa mtendaji  wa kata hiyo,  Joseph Bahegwa amesema hadi  jana saa 12 jioni hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.

Zakaria ameacha mke na watoto watatu.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz