Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushahidi kesi ya viongozi Wetcu waanza kutolewa mahakamani

11598 Kesi+pic TanzaniaWeb

Tue, 17 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (Wetcu), imeanza kusikilizwa na mashahidi watatu upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora.

Katika kesi hiyo namba 2/2017 ya uhujumu uchumi, inawakabili aliyekuwa mwenyekiti wa Wetcu, Gabriel Mkandara na wenzake watano kwa tuhuma za kusababisha hasara ya Sh109 milioni.

Wengine ni meneja, John Kusanja; mhasibu, Prosper Mbacho; ofisa uhusiano, Hamza Kapera; ofisa masijala, Francis Penta; ofisa masijala: makamu mwenyekiti, Msafiri Said na mfanyabiashara Faras Abbas.

Wakiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Shedrack Kimaro mbele ya hakimu mkazi, Chiganga Mashauri, mashahidi Amin Mtowazo (kaimu meneja Wetcu), Ekwabi Steven Mganga kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Isaack Kasenso aliyekuwa mjumbe wa bodi ya Wetcu kwa nyakati tofauti walidai kuwa mrajisi ndiye mwenye mamlaka ya kuidhinisha ununuzi wa mali za ushirika.

Hivyo, bodi haiwezi kubadili uamuzi wa mkutano mkuu wa wanachama.

Viongozi hao walikamatwa Machi 16, 2017 kwa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipofanya ziara ya kikazi mkoani hapa.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka matano; kula njama, kughushi, matumizi mabaya ya ofisi, kufanya ununuzi bila kibali na kusababisha hasara kati ya Juni mosi hadi Julai 31, 2015.

Chanzo: mwananchi.co.tz