Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushahidi kesi ya mwalimu mkuu kumbaka, kumpa mimba mwanafunzi wake Agosti 26

72097 Pic+ushahidi

Tue, 20 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma Agosti 26, 2019 inatarajia kuanza kusikiliza ushahidi wa kesi ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyantole iliyopo wilaya ya Kigoma, Jason Rwekaza (42) anayetuhumiwa  kwa makosa saba.

Kati ya makosa hayo, sita ni ubakaji na moja kumpa mimba mwanafunzi wake wa darasa la tano.

Akizungumza leo Jumatatu Agosti 19, 2019 Wakili wa upande wa Serikali Clement Masua, mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Flora Mtalania amesema tayari imeandaa mashahidi watakaokwenda kutoa ushahidi mahakamani hapo pamoja na vielelezo viwili.

Amesema vielelezo hivyo ni pamoja na daftari la mahudhurio kutoka shule anayosoma mwanafunzi huyo pamoja na fomu ya polisi namba 3(PF3).

Awali wakili wa Serikali alisema mshtakiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti na kufanya mapenzi na mwanafunzi huyo mara sita.

Alisema mshtakiwa alimbaka mwanafunzi huyo kinyume na kifungu cha sheria 130 (1)(2)(e) na 131 (1) cha makosa ya jinai kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 na kosa la kumpa mimba mwanafunzi huyo kinyume cha kifungu cha 60 (a) kifungu kidogo cha (3)cha Sheria ya elimu namba 353 ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016.

Pia Soma

Kwa upande wake, wakili wa utetezi, Thomas Msasa aliiomba mahakama hiyo kutoa ruhusa mteja wake kupima vina saba (DNA), pindi mwanafunzi huyo atakapojifungua ili haki iweze kutendeka kwa pande zote wakati kesi ikiwa inaendelea.

 

 

Mshatakiwa alikana mashtaka yote saba na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 26, 2019 kwaajili ya kuanza kusikilizwa kwa mashahidi watatu wa mwanzo.

Chanzo: mwananchi.co.tz