Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushahidi kesi ya Zumaridi, wenzake waanza kusikilizwa

Zumaridi Pic Data Zumaridi amekosa dhamana hivyo kurudishwa rumande

Tue, 10 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diana Bundala maarufu 'Mfalme Zumaridi' na wenzake nane leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kusikiliza kesi inawayomkabili.

Shtaka hilo namba 11/2022 ambalo ni shambulio la kudhuru mwili linayomkabili kiongozi huyo na wenzake nane limeitwa kwa ajili ya kusikiliza ushahidi huku washtakiwa wakikabiliwa na makosa matatu ambayo ni kumshambulia ofisa wa Polisi, kuzuia ofisa wa Polisi kutekeleza jukumu lake na kumzuia ofisa wa umma kutekeleza wajibu wake.

Baada washtakiwa kufikishwa mahakamani mbele ya Hakimu, Monica Ndyekobora, upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Emmanuel Luvinga umemtambulisha shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni Ofisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Nyamagana, Christina Mwisongo (46).

Baada ya shahidi kujitambulisha Hakimu alimwagiza wakili wa Serikali, Emmanuel Luvinga kumuongoza shahidi huyo kutoa ushahidi wake huku upande wa Jamhuri ukianza kufanya hivyo.

Baada ya kuulizwa maswali na wakili wa Serikali, Hakimu alitoa nafasi kwa upande wa utetezi kumuuliza maswali shahidi hiyo.

Advertisement Baada ya pande zote kuuliza maswali hayo kwa saa 2:03, Hakimu aliamuru kesi hiyo iahirishwe kwa dakika 20 kuanzia saa 8:00 mchana huu.

Huu hapa mwenendo wa maswali na majibu katika kesi hiyo.

Katika mtiririko huu;

L: Inasimama kwa niaba ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Emmanuel Luvinga

Mawakili wa Utetezi ni

M: Erick Mutta

K: Steven Kitale

Ofisa Ustawi wa Jamii Nyamagana

C: Christina Mwisongo

Na

SS: Kwa niaba ya mtoto aliyetakiwa kuchukuliwa

Endelea....

Luvinga: Uko ndani ya mahakama kwa ajili ya kutoa ushahidi, mbele yako yupo hakimu na washtakiwa wapo.

Ongea kwa vituo, usiongee kwa spidi hakimu akashindwa kuelewa

Luvinga: unafanya kazi gani?

C: Ofisa Ustawi wa Jamii Jiji la Mwanza

L: Ofisi yenu iko wapi?

C: Mtaa wa Nela kata ya Isamiloo

L: Ofisi yenu inahudhunisha na nini?

C: Kulinda na kutetea haki za watoto kwa kushirikiana na wadau wanaojihusisha na masuala ya watoto

Vile vile tunahusika na kuchukua hatua zinazostahili katika kumuokoa mtoto anapokuwa katika mazingira hatarishi ili asipate madhara

Vile vile, ofisi yetu inahusika na kupokea na kutekeleza amri zote za mahakama zinazohusu kulinda haki na ustawi wa watoto katika madai ya kesi za Watoto zilizofikishwa mahakamani

L: Katika kutekeleza amri hizo za mahakama huwa mnashirikiana na kina nani?

C: Tunashirikiana na wadau mbalimbali wa ulinzi watoto hususani ni Jeshi la Polisi

L: Unaweza kukumbuka jambo gani Tarehe 22/2/2023

Hakimu: Mtoto anatakiwa alindwe kwa taratibu za kimahakama hivyo ukifikia kumtaja utaje SS

C: Jambo ninalokumbuka mchana nikiwa Ofisini alikuja wakili Linus Munishi akiwa ameambatana na Ally Shabani (Baba wa mtoto SS)

L: Walofika wakiwa na jambo gani?

C: Wakiwa wameleta amri ya mahakama iliyokuwa imetoa amri ya Ofisa Ustawi wa Jamii kwenda kumchukua mtoto

Pia nakala ya hukumu ya kesi ya madai namba 28/2020 iliyofunguliwa katika mahakama ya mwanzo ya Mkuyuni

L: Baada ya kuja na nyaraka walikuwa wakitaka hatua gani zichukuliwe na ofisi yenu?

C: Ofisi yetu ya Ustwi wa Jamii ilitekeleza amri ya mahakama ya kumchuku mtoto, hivyo ofisa ustawi wa Wilaya alinikabidhi jukumu la kufanya ufuatiliaji na kutekeleza amri ya mahakama hiyo

L: Alifika na vitu gani

C: Nakala ya talaka

Na amri ya mahakama ikimtaka ofisa ustawi wa jamii akamchukue mtoto SS

L: Unaweza kuitambuaje hiyo nakala ya hukumu

C: Naweza kuotambua kwa sababu ilikuwa imeandika anuani ya mahakama ya mwanzo Mkuyuni wilaya ya Nyamagana na madai ya takaka namba 38/2020

Vile vile ilikuwa na jina la Mdai lilioandikwa kama Ally Abbas Shaban na jina la Mdaiwa, Suzana Simon Douglas

L: Amri ilivyoelekezwa unaweza kuitambuaje

C: Upande wa kulia ilikuwa na anuani ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Mkuyuni wilaya ya Nyamaganau

Upande wa kushoto iliandika madai ya talaka namba 38/2020

Kwa chini iliandika anuani ya Ofisa ustawi wa Jamii Wilaya ya Nyamagana Mwanza

Kichwa cha habari Yah: Kumchukua Mtoto

Chini yake kulikuwa na sahihi ya hakimu na mhuri wa mahakama ya Mwanzo ya Mkuyuni

Baada ya kuipokea niliandika mawasiliano na wakili Linus na namba za simu za Ally Abbasi kwa kalamu ya wino wa bluu

(Anaonyeshwa karatasi na kutaja nakala ya hukumu ya shauri la madai namba 38/2020 kwa kuwa ina namba ya kesi na jina la mdai (Ally Abbas Shabani) na mdaiwa (Suzana Simon Daglas) na Amri ya mahakama ya kumchukua mtoto SS)

L: Ungependa tuifanyie nini mahakamani

C: Ningependa mahakama hii tukufu ipokee vielelezo hivi

 Hakimu: Upande wa utetezi? Kuna mapingamizi

(Kimya kinatawala, huku wakili wa utetezi wakisoma makabrasha)

Wakili wa Utetezi, Erick Mutta (M)

M: Mheshimiwa hatuna pingamizi

(Maelezo hayo yanachukuliwa na hakimu)

Hakimu: Mahakama inapokea hukumu ya shauri la talaka na barua ya tarehe 15/2/2022

Baada ya kupokea vielelezo hivyo shahidi unapewa usome vielelezo hivyo ili washtakiwa waweze kuelewe

C: (Anaisoma hukumu hiyo)

(Anasoma amri iliyoelekezwa na mahakama kwenye ofisi ya Ofisa Ustawi wa Jamii Jiji la Mwanza)

L: Baada ya kupokea nyaraka, unaweza ukakumbuka nini Februari 23, 2022

C: Siku hiyo mchana nilipigiwa simu na Ofisa wa Polisi aliyejitambulisha kama Mkuu wa Upelelezi Nyamagana, akinitaka nifike katika kituo cha Polisi Nyamagana, nilifaya hivyo nikaelekea kituo cha Polisi Nyamagana, nilipofika nilikuta Mkuu wa Upelelezi akiwa na askari watano (wa kiume wanne na wa kike mmoja), vile vile, nilimkuta wakili Linus akiwa na baba wa mtoto SS, Ally Abbas akiwa ameambatana na ndugu yake aitwae, Boniface

Baada ya hapo tulipewa maelekezo ya kwenda kumchukua mtoto SS kama amri ya mahakama ilivyoelekeza

Tulipanda gari ya Polisi wote kasoro Mkuu wa Upelelezi tukaelekea maeneo ya Buguku nyumbani kwa Zumaridi

Tulipofika gari ya Polisi ilipaki kwenye uzio wa nyumbani kwa Zumaridi, tukiwa tunashuka nyuma yetu akaja kijana mmoja akasema subirini niwafungulie geti

Baada ya kutueleza hivyo alisukuma geti aliingia ndani baadaya kuingia akafunga geti hilo akaenda mbele ambapo kulikuwa na duka hapo

Alipoelekea palikuwepo na watu wengine na nyumba

Mkuu wa msafara alisogeleea geti na kugonga akimtaka kijana huyo aje atufungulie, lakini hakuna aliyekuja kutufungulia

Tuliendelea kusubiri hapo lakini hakuna aliyekuja kutufungulia

Ndipo miongoni mwa askari tuliyekuwa naye alisema kwamba tuzunguke mbele kule kuna geti lingine linalotazamana na kibao cha shule ya msingi Holele,

Tulifika getini pale na tulikuta geti hilo liko wazi, hivyo tuliingia kupitia geti hilo na kuelekea alipokuwa yule kijana na watu wengine, tukakuta duka maana kulikuwa na caton za maji na vitu vingine

L: Weka vizuri ili mahakama iweze kukuelewa, eleza vizuri kwa nini mlienda kwa Zumaridi

C: Kutokana na taarifa za uchunguzi wa kijamiii ambazo mahakama iliamurimu ofisi ya afisa ustawi wa jamii tukapata taarifa kutoka kwa Baba aa mtoto SS alitueleza kwamba mtoto anaishi na mama yake Suzana Doglas kwa Zumaridi

C: Tulipofika pale miongoni mwa askari walienda kwenye geti ambalo kijana hakutaka kutufungulia akalifungua, dereva wa ile gari akaingiza ndani ya nyumba ya Zumaridi na akaegesha pale

C: Tukiwa pale wote kwa pamoja tuelekea kwa wale watu ambapo mimi niliona kama ni sehemu ya duka maana kulikuwa na bidhaa.

Kiongozi wa msafara, Afande Paulo, alijitambulisha na kututambulisha akieleza kwamba tunahitaji kuonana na Zumaridi

Baada ya kufanya hivyo, yule kijana alijibu kwamba hafahamu alipo hivyo hawakutupa ushirikiano wa kuonana na Zumaridi.

Mbele yetu kulikuwa na watu wengi wanaimba kwaya tukawafuata tukawafikia kiongozi wa msafara (Askari Paulo) aliwasalimia lakini waliendelea kuimba wala hawakuitikia salamu ndipo aliporudia kuwasemesha na kuwataka waache kuimba na watusikilize

Ndipo Afande Paulo alijitambulisha kwao kwamba sisi na maofisa wa Polisi tukiwa na ofisa ustawi wa jamii tunaomba kumuoma Zumaridi, tunaomba mtuelekeze alipo

Mwalimu wa kwaya alijibu akituambia kwamba yeye ni mwalimu wa kwaya tu amekuja kuwafundisha wanakwaya hivyo siyo msemaji mkuu, walitutaka turudi tulipotokea kwenye duka pale alipopataja kuwa ni mapokezi tukawaulize

Sisi tuliendelea kwenda mbele kwa sababu pale kulikuwa watu mbele pia kulikuwa na nyumba ya Zumaridi kwa hiyo tuliekea kwenye nyumba hiyo

Tulipofika kwenye ile nyumba kulikuwana watu wengi nje na ndani ambao tuliwakuta wako sebuleni wakiwa wanaume na wanawake, wanaume walivaa mashati meupe na suruali nyeusi na wanawake walivalia sare mashati meupe na sketi ndefu nyeusi

Watu wale walikuwa sebuleni tukaingia tuliwakuta wameshikana mikono wamesimama wakiwa wanasali kwa lugha ambao binafsi sikuielewa, hivyo tulisimama tukisbiri wamalize kusali tujiambulishe kwao ili tuwaeleze shida yetu, waliendelea kusali tukiwa tumesimama

Ghafla nilishikwa na mshangao watu wale walipoanza kuunguruma kama Simba ghafla anatetemeka na kuanguka chini, akianguka wenzake wanamsimamisha

Waliendelea hivyo kisha wakaanza kutembea wakiwa m wamenyoosha vidole na kutoa macho baada ya kuona hivyo tulitoka nje

L: Baada ya kutoka nje nini kiliendelea

C: Waliendelea kutufata wakinguruma vile na Zumaridi akiwepo pale

Walimkamata Afande James na kumuangusha chini wakaanza kumshambulia wakiwa wanamvuta huku na kule, kumkanyaga, wakimpiga mateke na kumkwaruza kwa makucha huku wakiwa wamemzingira

Tulishikwa na taharuki maana tulishindwa kumuokoa mwenzetu, hivyo alijitahudi kujiokoa lakini alishindwa

Baada ya kufanikiwa walipeana silaha na afande James wakihofia kwamba wanaweza kuporwa silaha ile ndipo alipofanikiwa kunyanyuka ndipo tuliooanza kusogea kwenye geti la kutokea

Hivyo tulishindwa kutekeleza agizo la mahakama, watu wale waliendelea kutufuatilia wakituzomea huku wakiturushia vitu mbalimbali ikiwemo kiti na dustbin na waumini waliokuwemo mule wakawa wananyanyuka na kuunguruma na kutufuza huku wakifanya vurugu

Waliendelea kutusindikiza hadi nje ya geti wakatufuata, dereva alivyoona tumefika pale akatoa gari nje ya geti, tukiwa pale nje ya geti tukaingia ndani ya gari ya polisi ambapo baba wa mtoto, Ally Abbas akanionyesha mama wa Mtoto SS, Suzan Doglas akiwa miongini mwa kundi lile wakituzomea

Tukaingia ndani ya gari tukawaacha wakiendelea kutuzomea.

L: Wakati yanatokea hayo ulimtambua nani?

C: Nilimtambua Zumaridi ambaye nimekuwa nikimuona kupitia matangazo yake yanayorushwa

Mwingine ni Suzana ambaye baba wa mtoto SS alinionyesha kuwa ni yule pale

(Anawanyoshea kidole Zumaridi na Suzana Simon Doglas)

Baada ya hapo dreva aliwasha gari tukaondoka eneo lile tukaelekea karibu na jengo la Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana tukaongea na mwenzetu aliyeshambuliwa (Afande James) ambaye alikuwa akitulaumu kwa kushindwa kumsaidia wakati alipokuwa akishambuliwa akasema ameumizwa na sisi tulimuona ana hali mbaya kwa sababu alionekana ana maumivu makali.

Afande James alisema anaenda kufungua kesi ya kushambuliwa na kuzuiwa kutimiza majukumu yake

Afande James tulimshusha njiani sisi tukaenda kituo cha kati Nyamagana tukaeleza kwamba tumeshindwa kutekeleza kazi tuliyoelekezwa na Mahakama.

M: Tunaomba tupatiwe vielelezo hivyo

M: Shahidi umeieleza mahakama ulipigiwa simu na Polisi kuitwa kituonu na ulipofika ulimkuta baba wa mtoto na wakili anayeitwa Linus, Je nu kweli?

C: Ni kweii

M: Aliyetoa agizo la kwenda kumchukua mtoto ni nani?

M: Tisaidie kuieleza Mahakama kwamba ulieleza mahakama kwamba una amri ya kutekeleza, Je uliipa Polisi taarifa kwamba una amri ya polisi ya kutekeleza?

C: Hapana, bali nilipigiwa simu na Polisi

M: Unakubaliana na mimi kwamba moja ya majukumu yako ni kuhakikisha jamii inaishi kwa amani, ni kweli au siyo kweli?

C: Ni kweli

M: Katika kuhakikisha jamii inaishi kwa amani katika utendaji wako wa kazi unapaswa kuutambua uongozi kuanzia ngazi ya kata hadi taifa, ni kweli au si kweli?

C: Ni kweli

M: Kwa kufany hivyo, unakubaliana na mimi kwamba utekelezaji wa amri hii nyumbani mlipoenda anapoishi mdaiwa, ulitakiwa kuutaarifu uongozi wa mtaa au kata kuwa mnaenda katika eneo hilo ni kweli au si kweli?

C: Ni kweli

M: Katika maelezo yako hakuna sehemu uliyoeleza kwamba mlitoa taarifa kwamba mkoa katika eneo hilo, je nu kweli au si kweli?

C: Ni kweli

M: Unakubaliana na mimi kwamba ofisa wa Serikali ni mtu mwenye akili timamu kwamba endapo ungetoa taarifa msingekutana na tukio hilo

C: Ni kweli

M: Katika mtiririko wa masimulizi yako, ni sehemu moja tu ulipoonyeshwa mama wa mtoto akishangilia ndani ni kweli au si kweli?

C: Ni kweli!

M: Tofauti na wakati huo, haukumuona akishiriki au kushangilia kweli au si kweli?

C: Anasitaaa na kuingiliwa na wakili wa Serikali huku akimuomba hakimu aamuru shahidi asishurutishwe kujibu kama wakili wa utetezi anavyotaka.

C: Miongini mwa waliokuwemo mule ndani ya nyumba na waliokuwa wanatuzomea ni Suzana, na nilitambua hivyo baada kuelekezwa na baba wa Mtoto

M: Baada ya tukio uliandikisha maelezo kituo cha Polisi?

C: Ndio

M: Ilikuwa tarehe gani?

C: Sikumbuki

M: Muda gani uliandikisha

C: Tuliitwa kati ya baada ya siku mbili tatu

M: Ukiona maelezo yako, utayatambua?

C; Ndiyo

M: Kwenye maelezo yako kuna sehemu uliyoeleza kuwa ulimuona Suzana Doglas

C: Ndiyo nilimueleza Askari wa Polisi aliyekuwa akiniandikisha maelezo, kama alisahau basi atakuwa alipitiwa

M: Baada ya kuandikishwa ulisomewa maelezo hayo

C: Ndiyo

M: Kuna mahala popote kwenye maelezo yako ulimtaja

C: Sikumbuki ila alikuwepo eneo la tukio

M; Kwenye maelezo yako umeeleza kwamba Zumaridi alikuwepo wakati wakisali

C: Alikuwepo

M: Kwa ushahidi ukiotoa, kuna mahala popote unetaja tukio alilotaja Zumaridi tifauti na kusali?

C: Lipo kwa sababu kati ya wale waliotufuata na yeye alikuwepo

M: Tueleze Zumaridi alimpiga sehemu gani ya mwili wake?

C: Walikuwa wanamshambulia Afande James sehemu mbalimbali kwa sababu walikuwa wakimshambulia kwa pamoja

M: Zumaridi alimshambulia Afande James kwa pigo gani?

C: Watu walikuwa wengi Mheshimiwa hivyo sikuelewa sehemu gani wanamshambulia, Mimi mwenyewe nilikuwa kwenye taharuki

M: Kwa hiyo haukuona au hauna kumbukumbu

C; Niliona

M; Eneo la tukio wakikuwepo watu wangapi?

C: Walikuwa wengi ndani na nje ya nyumba

M: Washtakiwa namba moja hadi nane, Je kuna yoyote uliyewahi kukutana naye awali kwenye maisha yako?

C: Hapana

M: Je Zumaridi umewahi kukutana naye wapi?

C: Nilikuwa nikimuona kwenye TV na kwenye matangazo yake

M: Mheshimiwa hakimu tunaomba maelezo aliyoandikishwa shahidi

M: Kwa mujibu wa kifungu cha 9 kidogo cha 3 cha Sheria ya Mwenendo wa makosa ya Jinai kinaturuhusu kuomba maelezo aliyoandikishwa Polisi.

Pia sheria ya ushahidi inatupatia haki ya kuomba ushahidi huo.

L: Kipengele hicho, kinaweza kutoa uhuru kuhusu taarifa inayohutajika inaweza kuripotiwa kwa maandishi au maelezo

M: Msingi wetu umejielekeza hapo, tunaomba tupatiwe maelezo aliyoandikishwa shahidi ili tuweze kuendelea tulipoishia.

Hakimu: Kwa mujibu wa Kifungu 9 kidogo cha 3 cha Sheria ya Mwenendo wa makosa ya Jinai muwapatie hayo maelezo

M: Shahidi ielewe mahakama kama nyaraka hii unaitambua

C: Nyaraka hii naitambua ni maelezo ambayo nilikuwa nikimueleza Askari wa Polisi

M: Mheshimiwa Hakimu Shahidi ameitambua nyaraka hiyo kuwa ni maelezo yake aliyoeleza Polisi

Hakimu anatia saini kwenye nyaraka hiyo.

M: Shahidi isaidie mahakama yako, kwa mujibu wa maelezo yako uliyoshika, ni wapi umeeleza humo kwamba umemuona Zumaridi akifanya ulichoeleza mwanzo akishambulia, akizomea na kupiga askari!

C: Nilieleza kwamba watu waliokuwepo wengi kwamba walitushambulia kwa pamoja

M: Ni wapi uliieleza Polisi kwamba umemuona Suzana alishambulia?

Hakimu: Shauri lililopo mahakamani ni Shambulio la kudhuru mwili kwa lengo la kuzuia Ofisa wa serikali kutekeleza majukumu yake kwa hiyo turejee kwenye misingi ya kutaka kuthibitisha kwenye hayo na itupeleke kwenye uhalisia wa jambo

C: Kwenye karatasi hii nilieleza japo sikumtaja jina ila nilisema Mama wa mtoto SS

M: Huoni kuna umuhimu wa mahakama ipokee maelezo hayo kama kielelezo cha kutumika kutoa hukumu

C: Ndiyo maana nimeomba hakimu aupokee

Wakili wa Utetezi, Kitale (K)

K: Ni kweli mlienda kwa Zumaridi tarehe 23/2/2022 ?

C; Ni kweli

K: Je tarehe hiyo hiyo mlirudi kituo cha Polisi kutoa mrejesho?

C: Ni kweli

M: Ni kweli baada ya kutoa taarifa hiyo, hukuchukuliwa maelezo yako hukuchukuliwa maelezo yoyote hadi ilipofika tarehe 25/2/2022

C: Maelezo ya kwamba nilizuiwa nilitoa Februari 23,2022 ila ya kuandika nikitoa tarehe  25/2/2022

K: Shahidi unaelimu gani?

C: Ninashahada ya Ustawi wa Jamii na Lishe ya Jamii

K: Nielezee majukumu yako kwa mujibu wa maelezo yako?

C (Anayataja)

K: Kwa hiyo ni kweli kabisa kwamba kwenye hii hukumu iliyotolewa haukuhusika kabisa

C: Kwenye hukumu hiyo sikuhusika alienda mwenzangu mimi sikuwepo, ila aliifanya mwenzangu

K: Je uliiona ripoti hiyo?

C: Binafsi sikuiona

K: Katika hiyo ripoti ni kweli kwamba yule Ofisa Ustawi Jamii alitembelea ile familia?

C: Kwa mujibu wake aliitembelea

K: Na alipoitembelea je aliitembelea kwa Zumaridi?

C: Hakusema ameitembelea wapi

K: Moja ya kazi ya Ofisa Ustawi wa Jamii ni kutembelea familia inapoishi sasa ilikuwaje wakaenda kwa Zumaridi badala ya kutembelea nyumbani kwa ile familia?

C: Mimi nilipewa maelekezo na baba wa mtoto kuwa mtoto wake yuko kwa Zumaridi

K: Kwa hiyo hukusoma ripoti ya mahakama?

C: Mimi nilifata maelekezo ya mahakama

K: Ni watu wangapi mliingia ndani kutumia huo mlango?

C: Mimi, afande Paulo, Afande James na wengine

K: Nimeuliza mlikuwa wangapi mlioingia kupitia huo mlango?

C: Sikumbuki

K: Ni watu wangapi walioingia kupitia mlango wa mbele baada ya mlango kufunguliwa ?

C: Ni gari ya Polisi

K: Ndani ya gari alikuwepo nani?

C: Simfahamu jina lake

K: Wakati mnashambukuwa nani alifungua geti ili mtoke nje?

C: Mimi nilikuwa nyuma sikuona aliyefungua

K: Kwa hiyo ni wazi kwamba ni watu wa mle ndani ndiyo waliowafungulia?

C: Sikumbuki

K: Mlipoelekezwa kwamba mkaulize kule juu mkaulize, je ni kweli mlikaidi maelekezo mliyopewa na yule kiongozi au siyo kweli?

C: Hatukuyafata maelekezo kwa sababu hawakutupa ushirikiano mwanzoni

K: Je wewe ulishambuliwa?

C: Kimya

K: Mtu gani mwingine aliyeshambuliwa?

C: Nilimshuhudia James akishambuliwa

K: Kati ya walioko hapa wanane ni yupi alikuwa akiwashambulia akirusha viti

C: Nahisi ni huyu

K: Mheshimiwa ameshindwa kumtambua aliyekuwa akimrushia viti, naomba iwekwe kwenye rekodi

K: Je huyo mtoto aliyekuwa ameshikiliwa ulimuona kwenye tukio?

C: Sikumuona

K: Wakati mnaondoka, huyu Afande aliyejeruhiwa mlimshushia wapi?

C: Tulimshusha kwa mbele?

K: Wapi?

C: Sikunote, ila ni karibu na kituo cha Igogo

K: Kwa hiyo ukimtoa yeye, wengine wote mlienda kituo cha Polisi Mwanza

C: Ndiyo

K: Askari walikuwa na silaha ngapi?

C: Nilizoziona mimi ni mbili

K: Aina ipi?

C: Bastora na nyingine siijui

K: Ni nani na nani walikuwa wanabadilishana?

C: Siyo kwamba walikuwa wanabadilishana, Afande James alimrushia afande Paulo ili wasije wakaichukua wakati anapigwa

K: Kwa nini yule Afande ndiyo aliyeshambuliwa na siyo ninyi wengine

C: kwa sababu yeye alikuwa ndiyo alikuwa wa kwanza kudakwa, wakaanza kumshambulia na kumwangusha chini wengine tukirudi nyuma

K: Umesema ni mfanyakazi wa Ustawi wa Jamii kwa miaka zaidi ya 15, wajibu wako ulipofika eneo la tukio ni upi?

C: Kutekeleza amri ya mahakama

K: Wewe ni Ofisa Ustawi wa Jamii, je wajibu wako ni upi pale?

C: Ni kuhakikisha namchukua mtoto na kumleta mahakamani ili akabidhiwe kwa baba yake

K: Ulitakiwa ufuate utaratibu upi ili kutekeleza amri hiyo?

C: Kwa sababu ni nyumbani kwa Zumaridi nilitakiwa kumfuata Zumaridi ili atuletee huyu mtoto

K: Kwa hiyo afande ndiyo alikuwa anazuiliwa na siyo wewe?

K: Kwa hiyo utakubaliana na mimi kwamba wewe hukujitambulisha?

C: Si kweli

Hakimu: Tunaahirisha kesi hii kwa dakika 20 tutarudi kuendelea kusikiliza ushahidi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live