Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushahidi kesi ya Bosi Mange Kimambi App Juni 1

F4230bb620c81bf48e83f2e9dff33182 Ushahidi kesi ya Bosi Mange Kimambi App Juni 1

Wed, 27 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam inatarajia kuanza kusikiliza ushahidi wa kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Mtandao wa U-turn unaoendesha App ya Mange Kimambi, Allen Mhina.

Ushahidi huo unatarajiwa kuanza kusikilizwa Juni 1, 2022, baada ya upande wa mashtaka kumsomea mshtakiwa huyo hoja za awali mahakamani hapo jana.

Akisoma hoja hizo mbele Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwanaamina Eddie, alidai washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mtandao wa U-turn na App ya Mange Kimambi.

Katika maelezo hayo alidai Mhina ni Mkurugunzi wa Mtandao wa mshtakiwa wa 2 (U-turn) na mshtakiwa wa 3 (App ya Mange Kimambi).

Alieleza kuwa U-turn imesajiliwa na Brella na inajishughulisha na kazi za ubunifu na burudani sambamba na kurusha maudhui ya mtandao kutokana na leseni waliyoipata kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Alidai kwa kutumia leseni hiyo iliyotolewa Septemba 22, 2020 kwa pamoja mshtakiwa Allen na Mtandao wa U-turn, wanahusika kuendesha shughuli zote za App ya Mange Kimambi, ambayo katika utendaji wake inategemea mtandao wa U-turn kukusanya mapato kupitia kampuni ya selcom.

Aliendelea kudai kuwa Machi 9, 2022 App ya Mange Kimambi ilichapisha video iliyoonesha mgonjwa aliyekuwa amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Muhimbili ikiambatana na maneno:"PROFESA JAY AKIWA ICU. Hii ndiyo hali ya Profesa Jay kwa sasa tumuombee," ikiwa ni maudhui yenye kudhalilisha na kukiuka haki ya faragha.

"Mheshimiwa kutokana na maudhui hayo, upelelezi wa polisi ulifanyika kubaini nani mhusika, baada ya hapo mshtakiwa wa kwanza alikamatwa na kuhojiwa na katika maelezo yake ya onyo alikubali kwamba yeye ni Mkurugenzi wa mshtakiwa wa 2 na 3, baadaye alifikishwa mahakamani kusomewa mashtaka," alisema Mwanaamina.

Baada ya kusomewa hoja hizo mshtakiwa Mhina alizikataa isipokuwa mambo mawili, kwamba yeye ni Mkurugenzi wa U-turn na alifikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka.

Katika ushahidi huo upande wa mashtaka ulidai kuwa unatarajia kuwa na mashahidi 15.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP) aliwasilisha mahakamani hapo hati ya maombi ya kuifunga akaunti ya mtandao wa U-turn iliyoko katika benki ya CRDB tawi la Azikiwe, hadi pale uchunguzi mwingine utakapokamilika maombi ambayo mahakama iliyaridhia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live