Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upepelezi haujakamilika kesi ya Hariri kusafirisha heroine

37026 Hariripic Upepelezi haujakamilika kesi ya Hariri kusafirisha heroine

Thu, 17 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kesi inayomkabili mfanyabiashara Hariri Mohamed Hariri ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin, upelelezi wake bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Ester Martine ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa.

Martine alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Mtega kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya  kutajwa.

Baada ya kusikiliza maelezo hayo Hakimu Mtega aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 28, 2019, itakapotajwa tena.

Katika kesi ya msingi, Hariri anadaiwa kutenda kosa hilo, Machi 2, 2018, maeneo ya Kinondoni Matitu, Dar es Salaam.

Mshtakiwa anadaiwa siku hiyo ya tukio, alikutwa akisafirisha gramu 214.11 za dawa za kulevya aina ya heroin.

Mshtakiwa amerudishwa rumande, kutokana na shtaka linalomkabili kutokuwa na dhamana.

Soma Zaidi: Jalada kesi ya mfanyabiashara Hariri lipo kwa DPP



Chanzo: mwananchi.co.tz