Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi wakamilika kesi ya mauaji inayomkabili askari wa JWTZ, mwenzake

Hukumu Pc Data Upelelezi wakamilika kesi ya mauaji inayomkabili askari wa JWTZ, mwenzake

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dar es Salaam. Serikali imesema upelelezi wa kesi ya mauaji inayomkabili askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na mfanya usafi wa SUMA JKT, umekamilika na sasa imewasilisha taarifa na nyaraka muhimu Mahakama Kuu ili kesi hiyo iweze kuendelea na hatua nyingine.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya mauaji namba 9/2023 ni MT 95534 Coplo Jacob Sylivester Sechonge (34) na mkazi wa Mwenge kambi ya Jeshi pamoja na Almas Seleman (26) mfanya usafi kutoka SUMA JKT na mkazi wa Buza.

Wakili wa Serikali, Roida Mwakamale ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Desemba 4, 2023 wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Mwakamale amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo kuwa shauri hilo limeitwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi umekamilika na tayari upande wa mashtaka wameshawasilisha taarifa muhimu Mahakama Kuu kwa ajili ya hatua nyingine ikiwemo washtakiwa kusomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo( Commital.

Mwasamale amedai kutokana na hali hiyo, anaomba mahakama ipange tarahe nyingine kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama taarifa hizo zimeshasajiliwa kwa ajili ya kuendelea na hatua nyingine ambayo ni washtakiwa kusomewa hoja za awali( PH).

Baada hayo, hakimu Mazengo aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 18, 2023 itakapotajwa.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 15, 2020 eneo la Fire, lililopo wilaya ya Ilala.

Inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio, washtakiwa wanaodaiwa kumuua mtu mmoja aitwaye Abdul Ahmed.

Washtakiwa wapo rumande kutokana na shtaka la mauaji linalowakabili, kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live