Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi wa makosa madogo kukamilika kwa miezi 6

IGGGP WEB Upelelezi wa makosa madogo kukamilika kwa miezi 6

Wed, 19 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa ili kuhakikisha wanapunguza mrundikano wa wafungwa mahabusu pamoja uchelewashwaji wa kesi wamekubaliana kwamba upelelezi wa makosa makubwa utachukua miaka miwili huku upelelezi wa kesi ndogo ukichukua miezi sita pekee.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 18, 2021, mkoani Dar es Salaam, wakati akiwasilisha hali ya usalama wa nchi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, mara baada ya kufungua kiwanda cha ushonaji cha jeshi hilo.

"Tumekubaliana kwamba lazima makosa makubwa tuwe tumekamilisha upelelezi kwa miaka miwili na makosa madogo angalau kwa miezi 6 tuwe tumekamilisha upelelezi, nikuhakikishie Mh. Rais kwamba suala la mrundikano mahabusu na uchelewashwaji wa kesi litaendelea kupungua", ameeleza IGP Sirro

Chanzo: eatv.tv