Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi mwanasheria IPTL bado haujakalimika miaka 5

Sheria Ya Uganda Dhidi Ya Wapenzi Wa Jinsia Moja Yapingwa Mahakamani Upelelezi mwanasheria IPTL bado haujakalimika miaka 5

Mon, 12 Jun 2023 Chanzo: Mwananchi

Kesi inayomkabili Mwanasheria wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege upelelezi wa shauri hilo haujakamilka kwa zaidi ya miaka mitano.

Makandege alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Desemba 20, 2019 na aliunganishwa na wenzake Habirnder Seth Singh na James Rugemalira akikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya dola za Kimarekani 980,000.

Wakili wa Serikali, Fatuma Waziri aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi bado haujakamilika.

"Upelelezi bado haujakamilka na tunaomba mahakama hii ihairishe shauri hili Kwa ajili ya kutajwa," alidai Waziri.

Hata hivyo Juni 21, 2021 Seth ambaye aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, Seth alikiri shtaka moja la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kati ya mashtaka 10 yaliyokuwa yakimkabili ambapo tisa alifutiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) na alikubali kulipa fidia ya Sh26.9 bilioni.

Pia mahakama hiyo ilimfutia mashtaka ya kujipatia fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow na kumuachilia huru Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemarila.

Hatua huyo imekuja baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya mshtakiwa huyo.

Hata hivyo Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi aliahirisha shauri hilo hadi Julai 11, 2023 kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi ya msingi kati ya Januari 23, 2014 na Februari 2014 alijipatia Dola 380,000 katika Benki ya Stanbic iliyopo Kinondoni na Dola 600,000 katika Benki ya UBL iliyopo wilayani Ilala, fedha zilizotoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa nyakati tofauti na kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 980,000.

Chanzo: Mwananchi