Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi ya wanaodaiwa kuiba njia ya mtandao haujakamilika

74107 Ushahidi+pic

Tue, 3 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa leo Jumanne Septemba 3, 2019 kuwa upelelezi wa kesi ya kutakatisha Sh154 milioni inayowakabili washtakiwa 13 umekamilika.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mitano, likiwemo la kuomba hela kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno(sms) kwa watu tofauti maarufu kama 'nitumie hela kwenye namba hii'.

Wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon ameeleza hayo leo wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi, Kelvin Mhina.

“Upelelezi wa kesi hii umekamilika hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasilisha nyaraka muhimu Mahakama Kuu," alidai Simon.

Hakimu Mhina baada ya kueleza hayo ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 17, 2019 kesi hiyo itakapotajwa.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi  namba 58/2018 ni Boniface Maombe, David Luvanda, Moshi Sungura, Amos Bosco, Lule Kadenge, Jofrey Kapangamwaka, William Nturo, Regius Mauka, Collins Mwang'omolan, Francis Kapalata, Kasonde Kapela, Enock Mwandaji na Pascal Kiatu.

Pia Soma

Advertisement   ?
Kwa pamoja  wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 6, 2018 katika Jiji la Dar es Salaam na mkoani  Rukwa na maeneo mengine ndani ya Tanzania.

Katika kipindi hicho, washtakiwa  walikula njama kwa kutuma meseji zisizotakiwa katika maeneo ya Dar es Salaam, Rukwa na sehemu zingine ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika shtaka la pili, washtakiwa  wanadaiwa kuchapisha taarifa za uongo zikiwa katika muundo wa jumbe fupi (SMS), kupitia mfumo wa kompyuta kwa nia ya kudanganya.

Pia wanadaiwa kusambaza Meseji za kielektroniki zisizotakiwa kupitia mfumo wa kompyuta.

Katika shtaka la nne , katika kipindi hicho kwa njia ya kudanganya na kushawishi, walisambaza ujumbe mfupi wa kielektroniki kwenda kwa watu tofauti tofauti wakionyesha kuwa wanayo mamlaka ya kufanya hivyo wakati si kweli.

Shtaka la tano wanadaiwa kati ya Machi na Juni 2018 mkoani Rukwa na katika maeneo ya Dar es Salaam na sehemu nyingine za Tanzania washtakiwa kwa pamoja walijihusisha na muamala wa Sh154,032, 830 huku wakijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz