Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi ya walimu wanaodaiwa kusamabaza mitihani la saba haujakamilika

Hukumu Pc Data Upelelezi kesi ya walimu wanaodaiwa kusamabaza mitihani la saba haujakamilika

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upelelezi wa kesi ya kusambaza mitihani ya Taifa ya darasa la saba kwa kutumia mitandao ya kijamii wa Telegram inayowakabili washtakiwa 12, wakiwemo walimu, bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Yusuph Aboud ameielezea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Jumatano Novemba 30, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo, wakati kesi hiyo ya jinai namba 159/2022 ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

"Mheshimiwa hakimu, kesi hii imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri hili bado unaendelea, hivyo tunaomba terehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," amedia Aboud.

Wakili Aboud baada ya kueleza hayo, Hakimu Pamela ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 5, 2023, itakapotajwa.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Jonson Ondieka (37), Elinanami Sarakikya(33), Joyce Nyanyakika(50), Llyoyd Mpande(32), Ronalda Odongo(31), Dorcas Muroso(50), Alcheraus Malinzi(47), Raphael Innocent, Jacob Adagi na Joel Naome wote ni walimu pamoja.

Wengine ni Patrick Chawana (42), Theresia Chitanda(37), ambao ni wafanyabiashara.

Washtakiwa hao wakikabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kuvujisha mitihani na kutengeneza nyaraka za uongo.

Katika mashtaka yao, mshtakiwa Malinzi inadaiwa kati ya Oktoba 2, 2022 na Oktoba 12, 2022 sehemu isiyojulikana mshtakiwa huyo akiwa na nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka za uongo wa mtihani wa somo la uraia la darasa la saba akijifanya mtihani huo ni halali na umeandaliwa na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).

Pia, tarehe hiyo na sehemu isiyojulikana mshtakiwa Malinzi akiwa na nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka za uongo wa mitihani wa somo la Maarifa ya Jamii wa darasa la saba uliijifanya mwaka 2022, alionyesha kuwa mtihani huo ni na umeandaliwa na Necta.

Katika shtaka lingine, mshtakiwa Adagi na Ngome wanakabiliwa na shtaka moja la kuvujisha mitihani ya Taifa ya darasa la saba, kinyume cha sheria.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Oktoba 19, 2022 wakikabiliwa na mashtaka hao.

Hata hivyo, washtakiwa hao wapo nje kwa dhamana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live