Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi ya wafanyakazi NSSF bado

82018 Pic+kesi+nssf Upelelezi kesi ya wafanyakazi NSSF bado

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upelelezi katika kesi inayowakabili wafanyakazi tisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) akiwemo kaimu mkurugenzi wa fedha , Jamila Vulu bado haujakamilika.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la utakatishaji wa fedha zaidi ya Sh2 bilioni.

SOMA ZAIDI:  Kilichojiri kesi ya vigogo wa NSSF

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Simon Wankyo alidai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

Naye wakili wa upande wa utetezi, Kungh'e Wabeya aliuomba upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi ili shauri hilo liweze kwenda mbele.

Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Kelvin Mhina aliahirisha shauri hilo hadi Novemba 7, 2019

Pia Soma

Advertisement
Mbali na Vulu wengine ni mhandishi wa hundi, Abdulrahaman Njozi, meneja uhakiki, Amiri Kapera, mhasibu mwandamizi, James Oigo, mhasibu mkuu, Hellen Peter, mhasibu kitengo cha madeni, Invonne Kimaro, mhasibu dawati la uchunguzi, Restiana Lukwaro, kaimu rasilimaliwatu, Tikyeba Alphonce na mhasibu, Dominic Mbwete.

Inadaiwa kuwa kati ya Julai Mosi, 2016 na Septemba 4, 2017 maeneo ya Dar es Salaam washtakiwa hao pamoja na watu wengine ambao hawapo mahakamani walikula njama na kutakatisha fedha kiasi cha zaidi ya Sh2 bilioni wakijaribu kuonyesha hundi hizo halali zimetolewa na bodi ya wadhamini ya NSSF huku wakijua si kweli.

SOMA ZAIDI:  Watumishi tisa NSSF akiwamo bosi wa fedha wapandishwa kortini

Katika shtaka la pili kati ya Julai Mosi, 2016 na Septemba 4, 2017 wakiwa katika ofisi za NSSF makao makuu Ilala, Dar es Salaam mshtakiwa Njozi na Kapera kwa nia ya kufanya udanganyifu walighushi hundi 47 za CRDB za akaunti namba ya bodi ya wadhamini ya NSSF.

Shtaka la tatu tarehe hiyo katika ofisi za NSSF makao makuu Ilala, Dar es Salaam, washtakiwa wote wakiwa watumishi wa umma walioajiriwa wanadaiwa kuiba zaidi ya Sh2 bilioni mali ya bodi ya wadhamini ya NSSF.

SOMA ZAIDI:  Watumishi tisa NSSF akiwamo bosi wa fedha wapandishwa kortini

Katika shtaka la nne tarehe hiyo hiyo katika ofisi za NSSF makao makuu Ilala, Dar es Salaam washtakiwa wote wakiwa watumishi wa umma waliisababishia hasara NSSF kiasi cha zaidi ya Sh2 bilioni kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Katika shtaka la mwisho tarehe hiyo hiyo katika ofisi za NSSF makao makuu Ilala, Dar es Salaam washtakiwa wote walijihusisha na mihamala haramu ya zaidi ya Sh2 bilioni huku wakifahamu fedha hizo ni mazalio ya kosa tangulizi.

SOMA ZAIDI:  Watumishi tisa NSSF akiwamo bosi wa fedha wapandishwa kortini

Chanzo: mwananchi.co.tz