Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi ya vigogo wa madini uko hatua za mwisho kukamilika

48564 Pic+karugendo

Mon, 25 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania (Tansort), Archard Kalugendo na Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu, uko hatua za mwisho kukamilika.

Wakili wa Serikali Wankyo Saimon amedai leo Jumatatu Machi 25, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaid upelelezi uko hatua za mwisho na jalada liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kusainiwa.

"Kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wa shauri hili uko hatua za mwisho na jalada liko ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kusubiri kusainiwa hivyo tunaomba tarehe nyingine," alidai Wakili Wankyo.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Shahidi ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 8, 2019 kwaajili ya kutajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na kesi ya uhujumu uchumi kutokuwa na dhamana.

Kalugendo na Rweyemamu ambao ni watumishi waa Wizara ya Madini, kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani hapo, Septemba 15, 2017, wakikabiliwa na  shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh2.4 bilioni.

Katika hati ya mashtaka, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na mkoani Shinyanga.

Kwa pamoja wakiwa wathaminishaji almasi wa Serikali na waajiriwa wa Wizara ya Madini, waliisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43 ambazo ni sawa na Sh2.4 bilioni.



Chanzo: mwananchi.co.tz