Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi ya vigogo TPA ‘kizungumkuti’

Kizungkjuti Vigogo Tpa.jpeg Upelelezi kesi ya vigogo TPA ‘kizungumkuti’

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upelelezi kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande (66) na wenzake watano, bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Caroline Materu, alieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Jumatatu Novemba 7, 2022 wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Kipande na wenzake hao wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Dola za Marekani 1.85milioni sawa na Sh 4.2.bilioni.

Wakili Materu ametoa meelezo hayo, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira. "Mheshiwa hakimu, kesi hii limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri hili bado haujakamilika, hivyo naomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa" amedai wakili Materu.

Kutokana na maelezo hayo, hakimu Regemalira aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 7, 2022 itakapotajwa na washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Oktoba 12, 2022 upande wa mashtaka ulieleza Mahakama kuwa jalada la shauri hilo mezani kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kupitiwa na kutolewa maamuzi.

Mbali na Kipande, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 39/2022 ni Peter Gawile (58) aliyekuwa Ofisa Rasilimali Watu wa TPA na mkazi wa Mianzini; Casmily Lujegi (65) mkazi wa Mbezi Juu na Mwenyekiti wa Bodi ya Manunuzi wa TPA, Mashaka Kisanta (59) Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi, Kilian Chale (51) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano pamoja na Andrew John.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 38/2022 wanadaiwa kati ya Oktoba Mosi, 2014 na Oktoba Mosi 2020 Dar es Salaam, walikula njama ya kutenda kosa la kuisababishia TPA hasara.

Shtaka la pili, kati ya Januari Mosi, 2015 hadi Februari 17, 2015 washitakiwa kwa pamoja wakiwa maofisa wa TPA, walitumia madaraka yao vibaya kwa kutangaza zabuni namba AE/016/2014-15/CTB/G/39 kwa nia ya kujipatia dola za Marekani 1,857,908.04 .

Shtaka la tatu, inadaiwa kati ya Oktoba Mosi 2014 na Oktoba Mosi, 2020 maeneo ya TPA na maeneo mengine ya Dar es Salaam, washtakiwa kwa makusudi walitangaza zabuni ya Enterprises Planning Resources (ERP) bila kupata kibali cha bodi ya zabuni ya mamlaka hiyo na kushindwa kufuata kanuni za zabuni hivyo kutoa malipo ya awali ya asilimia 40 bila idhini ya bodi hiyo, jambo lililosababisha TPA hasara ya Dola za Marekani 1.8milioni ambazo ni sawa na Sh 4.2 bilioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live