Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha 'bado ngoma mbichi'

Mfalme Wa Nigeria Apigwa Risasi Na Kufa Ndani Ya Kasri Upelelezi kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha 'bado ngoma mbichi'

Mon, 12 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upelelezi wa kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha na kumteka mfanyabiashara, inayomkabili Sufiani Kidevu (30) na wenzake wawili, bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Faraji Ngukah ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Juni 12, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ferdinand Kihwonde.

"Mheshimiwa hakimu, kesi hii imeitwa leo kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado tunaendelea nao, hivyo tunaomba terehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," amedai Ngukah.

Hakimu Kihwonde, baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka, ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 26, 2023 itakapotajwa.

Washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na shitaka la unyang'anyi wa kutumia silaha halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Mbali na Kidevu, ambaye ni mkazi wa Kizuka mkoani; washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai namba 85/2023 ni Celestini Kamuli (32) mkazi wa Kizuka na mfanyabiashara Husein Mwinyijuma (47) mkazi wa Gairo Magengeni, mkoani Morogoro.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Mei 17, 2023 katika Mtaa wa Zaramo na Jamhuri eneo la Posta jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, washitakiwa kwa pamoja wanadaiwa kuiba simu moja ya mkononi aina ya iPhone, mali ya Hussein Mohamed.

Kabla ya kutenda kosa hilo, washitakiwa wanadaiwa kumtishia Husein kwa bastola na kisha kumteka ili waweze kutekeleza wizi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live