Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi ya mauaji ya mwanaharakati wakamilika

Thu, 14 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar Es Salaam. Upelelezi wa kesi ya mauaji ya Wayne Lotter (52) inayowakabili mashtakiwa 17 wakiwemo raia wa Burundi, umekamilika.

Lotter alikuwa mkurugenzi na mwanzilishi mwenza wa shirika lisilo la kiserikali la Palms Foundation, aliuawa kwa kupigwa risasi Agosti 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selassie wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

Leo Jumatano Februari 13m 2019 wakili wa Serikali, Sada Mohamed ameieleza mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Sada amedai  mbele ya hakimu mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kwamba upande wa mashtaka unasubiri jalada la kesi hiyo lichapishwe kwa ajili ya taarifa muhimu.

"Kwa sasa upande wa mashtaka  tunasubiri jalada la kesi hii lichapishwe kwa ajili ya taarifa, hivyo tunaomba tarehe fupi  kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama jalada hili limeshakamilika kuchapwa" amedai Sada.

Hakimu Mhina baada ya kusikiliza hoja za pande zote,  ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 27, 2019.

Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la mauaji, wanatetewa na mawakili, Benedict Ishabakaki na Mluge Fabian.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya mauaji namba 19/2017 ni raia wawili wa  Burundi, Nduimana Jonas(40) maarufu Mchungaji na Bonimana Nyandwi.

Wengine ni Godfrey Salamba (42) mkazi wa Kinondoni Msisiri A, Inocent Kimaro (23) mkazi wa Temeke Mikoroshini, Chambie Ally (32) mkazi wa Kia/Boma na ofisa wa benki ya NBC, Robert Mwaipyana (31) mkazi wa Temeke Mikoroshini.

Meneja wa benki ya Backlays, Khalid Mwinyi (33) mkazi wa Mikocheni B; Rahma Almas (37) mkazi wa Mbagala B;  Mohammed Maganga (61) ambaye ni mchimba makaburi;  Allan Mafue, Ismail Mohammed, Leornad Makoye, Amino Sham, Ayoub Selemani, Joseph Lukoa, Gaudence Matemu na Abuu Mkingie,

Katika kesi ya msingi, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kati ya Julai Mosi na Agosti 16, 2017 walikula njama ya kufanya Lotter.

Katika shtaka la pili, washtakiwa hao wanadaiwa Agosti 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie iliyopo wilaya ya Kinondoni, wanadaiwa kumuua  Lotter.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz