Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi ya kutekwa Mo Dewji bado haujakamilika

77887 Pic+mo

Mon, 30 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upelelezi katika  kesi ya kutekwa  kwa Mfanyabiashara Mohammed Dewji  'Mo' ,bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali Daisy Makakala amedai hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na ameiomba  tarehe nyingine ya kutajwa.

Katika hatua nyingine wakili huyo alidai bado wanaendelea  kuwatafuta washtakiwa wengine ili waunganishe katika kesi hiyo.

Awali mahakama hiyo ilitoa hati ya kuwakamata washitakiwa hao ambao ni Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issac Tomo na Zacarious Junior wote raia wa Msumbiji na Phila Tshabalala ambaye ni raia wa Afrika Kusini.

Mmoja wa washtakiwa hao ambaye ameshafikishwa mahakamani hapo ni dereva wa taksi , mkazi wa Tegeta Mousa Twaleb.

Kesi hiyo imepangwa Oktoba 15 mwaka huu.

Pia Soma

Advertisement
Katika kesi hiyo inadaiwa Mei Mosi na Oktoba 10, 2018, katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam na Johannesburg Afrika Kusini, kwa makusudi washitakiwa wote kwa pamoja waliendesha genge la uhalifu.

Pia inadaiwa Oktoba 11, 2018 maeneo Hoteli ya Colloseum  wilayani Kinondoni Dar es Salaam, Twaleb pamoja na watu wengine ambao hawapo mahakamani, walimteka nyara MO kwa nia ya kumuhifadhi kwa siri na kumuweka maeneo ambayo ni hatari.

Pia inadaiwa Julai 10, 2018 maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Twaleb alitakatisha fedha ambazo ni Sh 8,000,000 wakati akijua fedha hizo ni kosa la kushiriki genge la uhalifu na makosa ya kupanga.

MO alitekwa nyara Oktoba 11, 2018 alfajiri maeneo ya Hoteli ya Colloseum wakati akienda kufanya mazoezi na alipatikana Oktoba 20, mwaka huo huo katika eneo la Gymkhana.

Soma zaidi: Watano kuongezwa kesi ya kutekwa Mo Dewji

Chanzo: mwananchi.co.tz