Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi ya Shamim, mumewe haujakamilika

60039 Pic+shamimu

Tue, 28 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili  mfanyabiashara, Abdul Nsembo maarufu Abdulkandida na mkewe, Shamim Mwasha umeomba upande wa mashtaka kuhakikisha unakamilisha upelelezi kwa wakati  ili kesi hiyo iweze kuendelea na hatua nyingine.

Nsembo na Shamim wakabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin.

Wakili wa utetezi, Hajra Mungula na Charles Kisoka  wametoa ombi hilo  leo  Jumatatu Mei 27, 2019 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Ombi hilo limetolewa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

“Kwa kuwa kesi hii haina dhamana na wateja wetu wanaendelea kusota rumande tunaomba upande wa mashtaka wajitahidi kukamilisha upelelezi kwa wakati ili kesi hii iweze kuendelea kwa hatua nyingine " amedai  Kisoka.

Awali, wakili wa Serikali, Simon Wankyo amedai shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Pia Soma

Hakimu Mhina baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote ameahirisha  kesi hiyo hadi Juni 10, 2019 itakapotajwa  tena na washtakiwa kurudishwa rumande.

Kwa mujibu  wa hati ya mashtaka, wawili hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 36/2019.

Wanadaiwa kwa kusafirisha  dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 232.70  wakati wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo Mei Mosi, 2019 katika eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Kwa mara  ya kwanza  washtakiwa hao walifikishwa Kisutu  Mei 13, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz