Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi ya Maxence Melo mpaka kwa DPP

86020 Pic+jamii+forum Upelelezi kesi ya Maxence Melo mpaka kwa DPP

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello na Micke William umedai wanawasiliana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kujua utaratibu wa upelelezi wa shauri hilo.

Wawili hao wanakabiliwa na kesi ya kuendesha mtandao ambao haujasajiliwa Tanzania kwa kikoa cha .co. tz (Tanzania domain).

Leo Jumanne Novemba 26, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakili wa Serikali, Adolf Lema amedai wanawasiliana na DPP kujua shauri hilo linaendaje kwa kuwa walikuwa na shahidi mmoja.

“Shauri lilikuja kwa ajili  ya kuendelea na usikilizwaji tunawasiliana na DPP kujua shauri hili linaendeleaje na shahidi aliyebaki ni mmoja,” amedai Lema.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ameahirisha shauri hilo hadi Desemba 12, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Katika Kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Desemba 9, 2011 na Desemba 13, 2016 katika eneo la Mikocheni, wilaya ya Kinondoni.

Wanadaiwa kuendesha mtandao huo  na kushindwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wa mtandao huo.

Chanzo: mwananchi.co.tz