Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi vigogo wa madini uko hatua za mwisho

46149 Pic+almaas Upelelezi kesi vigogo wa madini uko hatua za mwisho

Tue, 12 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili mkurugenzi wa uthaminishaji almasi na vito Tanzania  (Tansort), Archard Kalugendo na mthamini wa madini ya almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu uko hatua za mwisho kukamilika.

Wakili wa Serikali, Wankyo Saimon amedai leo Jumatatu Machi 11, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaid kuwa amefanya mawasiliano na mpelelezi wa kesi hiyo na kumwambia wako katika hatua za mwisho kukamilisha upelelezi.

"Kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wa shauri hili bado haujakamilika lakini nimefanya mawasiliano na mpelelezi amenihakikishia wako katika hatua za mwisho hivyo tunaomba tarehe nyingine," amedai Wakili Wankyo.

Wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko alidai kuwa tarehe hiyo wanataka wapate majibu kwa kuwa suala la kukamilika kwa upelelezi wameliomba kwa muda mrefu.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba, ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 25, 2019 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kwa kuwa kesi ya uhujumu uchumi haina dhamana.

Washitakiwa ambao ni watumishi kutoka Wizara ya Madini, kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani hapo, Septemba 15, 2017, wakikabiliwa na shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh2.4 bilioni.

Katika hati ya mashtaka, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na mkoani Shinyanga.

Kwa pamoja wakiwa wathaminishaji wa almasi wa Serikali na waajiriwa wa wizara ya  Nishati na Madini, waliisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43  ambazo ni sawa na Sh2.4bilion.



Chanzo: mwananchi.co.tz