Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi anayedaiwa kumuua mkewe, kumchoma kwa mkaa wakamlika

81088 Pic+jalada Upelelezi kesi anayedaiwa kumuua mkewe, kumchoma kwa mkaa wakamlika

Mon, 21 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili Mfanyabiashara Hamis Said (38) umedai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na jalada la shauri hilo lipo kwenye hatua ya uchapaji.

Wakili  wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai hayo leo Jumatatu Oktoba 21, 2019 mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi umekamilika.

Simon amedai jalada la shauri hilo lipo kwenye hatua ya uchapaji kwa ajili ya maandalizi ili lipelekwe Mahakama Kuu ya Tanzania hivyo ameiomba mahakama hiyo ihairishe kesi hiyo.

SOMA ZAIDI: Anayedaiwa kumuua mkewe, kumchoma moto ataka fedha zake kwenye simu

 

Hakimu Mkazi Mkuu, Salum Ally aliahirisha shauri hilo hadi Novemba 4, 2019.

Pia Soma

Advertisement
Katika kesi ya msingi mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la mauaji ambapo anadaiwa  Mei 15, 2019 katika oneo la Geza Ulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mtu anayeitwa Naomi Marajani kisha kumchoma kwa mkaa na mabaki kwenda kuyazika Mkuranga mkoani Pwani.

SOMA ZAIDI: Anayedaiwa kumuua mkewe kisha kumchoma moto awatolea uvivu waandishi wa habari mahakamani

Chanzo: mwananchi.co.tz