Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi anayedaiwa kumteka Mo Dewji haujakamilika

62211 Modewjipic

Wed, 12 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upelelezi wa kesi ya kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohamed Dewji ‘Mo’ inayomkabili dereva teksi, Mousa Twaleb haujakamilika.

Wakili wa Serikali Daiys Makakala amedai leo Jumanne Julai 11,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine.

Baada ya maelezo hayo hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 25, 2019 na mshtakiwa huyo kurejeshwa rumande.

Twaleb  anakabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kumteka nyara Mo.

Mo alitekwa Oktoba 11, 2018  maeneo ya Hoteli ya Colosseum alikokwenda kufanya mazoezi na kupatikana siku tisa baadaye baada ya watekaji kumtelekeza katika viwanja vya Gymkhana.

Habari zinazohusiana na hii

Chanzo: mwananchi.co.tz