Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upande wa utetezi kesi ya almasi wahoji upelelezi kutokamilika

80728 Utetezi+pic Upande wa utetezi kesi ya almasi wahoji upelelezi kutokamilika

Fri, 18 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa utetezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa mkurugenzi wa uthaminishaji almasi, Archard Kalugendo na mwenzake umedai wateja wao wapo ndani kwa zaidi ya miaka miwili lakini upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Oktoba 18, 2019 na wakili wa Serikali, Aldof Lema katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akieleza kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo anaiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine ya kutajwa.

Wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko amedai miaka miwili  imepita upande wa mashtaka unadai upelelezi haujakamilika.

"Kesi ipo kwa zaidi ya miaka miwili upelelezi wake haujakamilika na wateja wetu walishaandika barua ya kuomba dhamana  kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) lakini aliwandikia  hati ya kuwakatalia, sasa wafanyeje wapo ndani  kama vile wameshahukumiwa," amedai Nkoko.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ameahirisha shauri hilo hadi Novemba Mosi, 2019.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka,  washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga.

Pia Soma

Advertisement

Kwa pamoja na kwa vitendo viovu wakiwa wathaminishaji wa almasi wa Serikali na waajiriwa wa wizara ya Madini na Nishati, waliisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43  ambazo ni sawa na Sh2.4 bilioni.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz