Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upande wa utetezi kesi ya Mbowe wapinga Ushahidi wa ODC Kingai

Kupinga Onyoopic Upande wa utetezi kesi ya Mbowe wapinga ushaidi wa OCD

Wed, 15 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upande wa utetezi katika kesi ya kula njama na kutoa fedha kwa ajili ya kusiadia vitendo vya kigaidi inayomkabili, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wamepinga maelezo ya onyo yaliyotolewa na shahidi kwa kwanza katika kesi hiyo.

Wamesema kuwa Maelezo yasipokelewe kama kielelezo na Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, kwa sababu yamechukuliwa nje ya muda.

Maelezo hayo yametolewa leo Jumatano, Septemba 15, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Ramadhani Kingai wakati akitoa ushahidi dhidi ya washtakiwa hao.

Aidha kesi hiyo imesimama kwa muda hadi saa 8 mchana kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi ndogo kuhusu utaratibu wa utoaji wa maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili Adamu Kasekwa baada ya mawakili wake kuyapinga wakidai kuwa aliyatoa baada ya kuteswa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live