Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upande wa utetezi kesi ya Kisena na wenzake wahoji upelelezi kutokamilika

60120 Pic+kisena

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa utetezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Usafirishaji wa Mabasi yaendayo haraka, maarufu mwendokasi (Udart), Robert Kisena na mkewe, Frorencia Mshauri Membe na wenzao watatu wameuomba upande wa mashtaka uwaeleze ni lini watakuwa wamekamilisha  upelelezi wa shauri hilo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kulwa Kisena (33), Charles Newe (47) na Chen Shi (32).

Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa Serikali, Wankyo Simon kuieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Mei 28, 2019 kuwa upelelezi bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

"Hii kesi ndiyo kwanza ina mwezi mmoja tangu iunganishwe ina sehemu nyingi inafanyiwa upelelezi hivyo hatuwezi kusema ni lini au mwezi gani utakuwa umekamilika tutakuwa hatutendi haki kwa wenzetu," amedai Simon.

Wakili wa upande wa utetezi,  Zuri'el Kanzungu amedai kuwa upande wa mashtaka wanatakiwa kuieleza mahakama upelelezi umefikia wapi.

"Tunaomba upelelezi ukamilike kwa haraka ili shauri kumalizika haraka," amedai Kazungu.

Pia Soma

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile ameahirisha shauri hilo hadi Juni 6,2019 itakapotajwa tena na washtakiwa wamerudishwa rumande.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi 2011 na Mei 31,2018 katika maeneo tofauti wakiwa na watu wengine waliratibu shughuli za kihalifu huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Katika shtaka la pili kati ya Januari Mosi ,2015 na Desemba 31,2017 katika eneo la Jangwani washtakiwa Robert, Kulwa, Frorencia wakiwa mkurugenzi wa kampuni ya Zenon Oil Gas Limited alijenga kituo cha mafuta kinachoitwa Zenon Oil and Gas katika karakana ya kampuni ya Udart bila ya kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma na Nishati na Maji (Ewura).

Shtaka la tatu kati ya Januari Mosi, 2015 na Desemba 31, 2017 katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam washtakiwa hao wakiwa wakurugenzi wa kampuni hiyo kwa pamoja walianzisha biashara ya kuuza mafuta ya petroli katika eneo ambalo halijaruhusiwa.

Katika shtaka la nne la utakatishaji, kati ya Mei 25, 2015 na Decembe 31, 2015 wakiwa jijini Dar es Salaam washtakiwa hao waliibia Sh1,216,145,374 mali ya kampuni ya UDART.

Shtaka la tano la utakatishaji fedha, inadaiwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 katika jiji la Dar es Salaam washtakiwa Robert, Kulwa, Charles na Frolencia wakiwa na lengo la kuficha uhalisia walibadilisha thamani ya mafuta kuwa fedha yenye thamani ya Sh1, 216, 145, 374 kwa kuyauza wakati akijua mafuta hayo ni zao la uhalifu.

Pia,  shtaka la sita ni utakatishaji wa fedha washtakiwa hao wanadaiwa kuwa ambapo kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 wakiwa jijini Dar es Salaam waliweza kumiliki kiasi cha fedha hizo Sh1.216, 145, 374 huku wakijua ni zao la kosa la wizi.

Katika kosa la saba inadaiwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 akiwa jijini Dar es Salaam kwa makusudi aliisababishia hasara UDART ya Sh2.414, 326, 260.70.

Katika kosa la utakatishaji fedha linamkabili Robert Kisena na Chen Shi ambapo wanadaiwa Aprili 8, 2016 katika benki ya NMB,  Kisena akiwa Mkurugenzi wa UDART alihamisha Sh594.92 milioni kwenda kwenye akaunti nyingine ya kampuni ya Longway Engineering Company wakati akijua fedha hizo ni zao haramu lililotokana na makosa ya kughushi.

Katika kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu linalomkabili Kisena na Shi ambapo wanadaiwa walilitenda June 9, 2016 katika tawi la NMB Ilala ambako kwa nia ovu waijipatia Sh603.25 milioni kutoka Udart kwa kuonyesha kiwango hicho kimelipwa kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa Kituo cha Udart Kimara, Ferry (Kivukoni), Ubungo na Morocco

Chanzo: mwananchi.co.tz