Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upande wa mashtaka kesi ya Dk Tenga waomba muda zaidi

Fri, 26 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili  vigogo wa kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms, akiwemo Dk Ringo Tenga umeomba wiki mbili kukamilisha ukusanyaji wa vielelezo kabla ya kuhamishiwa Mahakama Kuu kitengo cha uhujumu uchumi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Hafidh Shamte na Peter Noni.

Wakili wa Serikali mwandamizi,  Wankyo  Symon amedai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Ijumaa Julai 26, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,  Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Wakili Wankyo amedai upelelezi wa shauri hilo umeshakamilika na wapo katika hatua za mwisho za ukusanyaji wa nyaraka hizo kuomba iahirishwe mpaka baada ya wiki mbili.

Wakili wa utetezi, Brayson Shayo alikubaliana na ombi hilo kwani watapata muda wa kushauriana na wateja wao.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 9 mwaka huu itakapotajwa tena.

Pia Soma

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka sita ikiwemo ya utakatishaji fedha.

atika kesi ya msingi, Dk Ringo ambaye ni Mkurugenzi na Mwanasheria wa kampuni hiyo na wenzake wanadai kuwa, kati ya Januari 1, 2014 na Januari 14,2016 Dar es Salaam, walitoza malipo ya mawasiliano ya simu za kimataifa  chini ya kiwango cha Dola za Marekani  0.25 kwa  dakika kwa lengo la kujipatia faida.

Pia katika kipindi hicho, wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA) kwa kutoza gharama chini ya kiwango na kushindwa kulipa kiasi cha Dola za Marekani 3,282,741.12 kwa TCRA, kama malipo ya mapato.

Washtakiwa hao , wanadaiwa  katika kipindi hicho  walishindwa kulipa ada za udhibiti za Dola za Marekani 466,010.07 kwa TCRA.

Dk Tenga  na wenzake wanadai kuwa, kati ya Januari 1, 2014 na Januari 14,2016 maeneo ya Dar es Salaam, walitoza malipo ya mawasiliano ya simu za kimataifa chini ya kiwango cha Dola 0.25 za Marekani kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida kinyume cha sheria.

Pia katika kipindi hicho wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutoza gharama chini ya kiwango na kushindwa kulipa Dola 3,282,741.12 za Marekani kwa TCRA kama malipo ya mapato.

Washtakiwa hao wanadaiwa katika kipindi hicho walishindwa kulipa ada za udhibiti za Dola 466,010.07 za Marekani kwa TCRA.

Katika shtaka la utakatishaji wa fedha, Hafidhi, Noni, Dk Tenga na Chacha wanadaiwa kuwa, walitumia ama walisimamia Dola 3,282,741.12 za Marekani wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya udanganyifu linalotokana na mashitaka yaliyotangulia.

Vile vile, washitakiwa hao wanadaiwa kuwa waliisababishia TCRA hasara ya Dola  3,748,751.22 za Marekani (sawa na Sh. 8 bilioni ).

Chanzo: mwananchi.co.tz