Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unyama! Vijana 4 wadaiwa kumbaka mwanafunzi wa uuguzi, wafungulia muziki mzito!

Rape ED Unyama! Vijana 4 wadaiwa kumbaka mwanafunzi wa uuguzi, wafungulia muziki mzito!

Wed, 13 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi l Polisi mkoani Kigoma linawashikilia watuhumiwa watatu kwa tuhuma za kumbaka msichana mmoja mwenye umri wa miaka 19, ambaye ni wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Tanga mwaka wa kwanza ambaye inaelezwa alibakwa kwa nguvu na vijana wanne.

Kamanda wa Polisi Kigoma, Ramadhani Kingai amesema tukio hilo limetokea katika eneo la Mrusi, Kata ya Heruchuni wilayani Kasulu ambapo vijana hao wanadaiwa walimkamata mhanga kwa nguvu na kuingizwa ndani ya nyumba kisha kumfanyia unyama huo huku wakifungulia redio kwa sauti kubwa.

"Mmoja ya watuhumiwa aitwaye Bakari Hassani alikula njama na wenzake, walivyokaribia kwenye nyumba ambayo anaishi binti huyo walimkamata na kumuingiza kwenye nyumba waliyomfanyia ubakaji huku wakiwa wamefungulia redio kwa sauti kubwa ili kelele za binti kuomba msaada zisisikike, walipomaliza walikimbia," amesema RPC Kingai.

Aidhq, RPC Kingai amewataja watuhumiwa kuwa ni Julius Yolemino (24), Hemed Miosho (24) na Bakari Hassani(21) na mtuhumiwa wa nne ambaye anafahamika kwa sura na aliyebakwa na bado anasakwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live