Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulinzi waimarishwa kesi ya kina Mbowe

Sun, 3 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ulinzi umeimarishwa katika eneo la Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam wakati kesi ya rufaa ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ikiendelea.

Askari polisi wamesambaa katika eneo la Mahakama hiyo huku magari yao matatu yakiwa yameegeshwa katika pande tatu, kulia kushoto na mbele ya lango la kuingilia Mahakamani hapo.

Tofauti na wakati mwingine ambapo wanachama hujitokeza kwa wingi, leo hali ni tofauti, hakuna wafuasi wa Chadema waliokaa nje ya lango la kuingilia Mahakamani hapo wala barabarani.

Askari magereza watatu wenye silaha wameonekana pia wakiwa juu ya jengo la Mahakama (ghorofa ya kwanza) wakitembea tembea na kuangaza huku na kule.

"Hawa jamaa (askari polisi) leo wamejipanga sana, wasingekuwepo hapa leo nisingefanya biashara kabisa maana wangeanza kupambana na wana-Chadema, tungeondolewa hapa," amesema Rajab Nengwe ambaye anauza machungwa kandokando ya barabara karibu na Mahakama Kuu.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz