Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulinzi shirikishi wawakimbiza wanaume ‘teleza’ Kigoma

62337 Terezapic

Wed, 12 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Bila shaka umeshasikia habari za wanaume wanaojipaka oil chafu ‘wanaume teleza’ kisha kuwabaka wanawake mkoani Kigoma, vitendo hivyo viliwafanya wananchi kuanza ulinzi shirikishi lengo likiwa ni kuwasaka na kuwafikisha katika vyombo vya Dola.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Juni 12, 2019, diwani wa Mwanga Kusini, Musa Maulidi amesema tangu Mei 19, 2019 hakuna tukio lililofanywa na wanaume hao kutokana na kuanza kwa ulinzi shirikishi kwa wananchi kushirikiana na polisi.

"Tangu tuanze ulinzi shirikishi hakuna tukio lolote la ubakaji lililotokea hadi sasa na hofu ya kuwepo vijana wa teleza imeanza kutoweka, kwa sasa amani ipo ya kutosha," amesema Maulidi.

Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kwenda mahakamani kutoa ushahidi kwa kuwa ni wanaume wanaowafahamu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno amesema jeshi hilo linaendelea na operesheni ya kuwakamata wahuni wote wakiwemo wanaume ‘teleza’.

Amesema wanawasaka wahuni hao ili kudumisha amani huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa polisi ili wahusika hao wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

Habari zinazohusiana na hii



Chanzo: mwananchi.co.tz