Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukioa mwanafunzi aliyeacha shule haya yatakukuta

32904 Mwnaafunzipic Tanzania Web Photo

Sat, 22 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nyang’hwale. Kama wewe ni mkazi wa Wilaya ya Nyang’hwale na unafikiri ukimuoa mwanafunzi aliyeacha shule baada ya kupata ujauzito utakuwa salama hakika utakuwa unajidanganya.

Ni kwa sababu wilaya hiyo sasa imeweka utaratibu wa kupima vinasaba kati ya mtoto na mwanaume aliyemuoa mwanafunzi  ili kubaini kama ndie baba halisi wa mtoto huyo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Hatua hiyo imekuja kutokana na wanafunzi wanaoacha shule baada ya kupata ujauzito kukataa kuwataja wanaowapa mimba lakini baada ya kujifungua huolewa  na kudai aliyewaoa sio baba wa mtoto.

Katika kipindi cha miaka mitatu wanafunzi 160 katika Wilaya hiyo wamepata ujauzito.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Desemba 22, 2018 mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale  Hamimu Gwiyama amesema Serikali imeamua kuwasaka wanafunzi walioolewa ili kubaini kama wanaume hao ndio waliokatisha ndoto zao za masomo.

“Wanafunzi wengi waliopata mimba sasa wameolewa lakini wanapohojiwa kujua aliyewapa mimba wanadai hawamjui au hawamkumbuki,” amesema.

“Sasa polisi watafanya uchunguzi na kuwahoji wote wawili kujua ukweli. Ikiwa hatutabaini tutawapima vinasaba  ikibainika ndio wahusika lazima sheria kali ichukuliwe  tunataka kumaliza tatizo hili kabisa.”

Gwiyama amesema kutokana na uwepo wa waraka wa elimu namba 5 wa mwaka 2011 unaoruhusu mwanafunzi kufukuzwa shule baada ya kuwa mtoro kwa  siku 90, imechangia wazazi wengi kuwakatisha masomo wanafunzi na kuwaoza.

“Tumeanza operesheni ya kuwasaka wote walioacha shule, haijalishi ni baada ya miaka mingapi bali wote walioacha shule tutawachukulia hatua lengo la operesheni hii ni kumaliza tatizo la mimba. Tuwajengee hofu wanaume wanaooa  wanafunzi” amesema.

Takwimu zinaonyesha  mwaka 2017 wanafunzi 170 wa sekondari waliacha shule kwa kupata ujauzito huku  90 wa shule za msingi wakishindwa kuendelea na masomo baada ya kupata ujauzito.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz