Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukatili: Amuua Mpenzi Wake na Mtoto Kisa Elfu 80

Fisi Mauaji?fit=613%2C356&ssl=1 Ukatili: Amuua Mpenzi Wake na Mtoto Kisa Elfu 80

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mkoani Geita, Mwanamume aliyemuua mpenzi wake baada ya familia kushindwa kumlipa pesa alizotumia kumtunza baada ya kuwekeana nadhiri ya ndoa pia anatuhumiwa kumuua mtoto wa mwanamke huyo, Winfrida Masumbuko (13).

Mwanamume huyo Peter John, mwishoni mwa Juni mwaka huu alishtakiwa kwa kumuua mpenzi wake, Ester John (28) mkazi wa Ibamba baada ya kudai kiasi cha pesa kilichokadiriwa Sh80, 000 aluzokuwa akimpa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe aliwaambia waandishi wa habari: “Mama (Esther John) alikuwa ameolewa na ana watoto watano, lakini mumewe alifariki Julai mwaka jana.

Inasemekana kuwa baada ya kufiwa na mumewe, alianza uhusiano na mtuhumiwa kwa hivyo alikua akimpa pesa kidogo ambayo wakati tunamuhoji alisema zilikuwa ni 80, 000.”

Aliendelea kusema kuwa mtuhumiwa alimteka nyara mwanamke huyo na mtoto wake baada ya kuwarubuni kwenda shambani kuvuna mpunga na alipofika hapo walimwacha mtoto na wakaendelea mbele ambapo mtu huyo alimuua mpenzi wake.

Kamanda Mwaibambe katika mahojiano na mtuhumiwa alikiri kuua na kwenda kuwaonyesha mahali alipomzika mpenzi wake na jeshi liliendelea na uchunguzi.

Kamanda Mwaibambe pia alisema mtuhumiwa alikiri kumuua mtoto wa mpenzi wake na kisha akatupa mwili wake vichakani na kukubali kuwapeleka polisi porini na kupata mabaki ya mwili wake ikiwemo kichwa na baadhi ya sehemu za mwili na nguo ya mtoto.

Wakati huo huo, Kamanda Mwaibambe alisema katika tukio lingine watoto wawili walipoteza maisha na wengine 15 walinusurika kifo baada ya kula chakula kinachoshukiwa kuwa na sumu.

Aliwataja waliokufa kuwa ni Manyirizu Joseph (6) na Berta Mateso (5) wote wakazi wa Ikobe wilayani Mbogwe. Kamanda Mwaibambe alisema watoto na majeruhi walikula mabaki ya chakula (uji) ambao ni mchele na kondo la nyama na kuanza kutapika na kuharisha.

Alisema manusura bado wanapata matibabu katika kituo cha afya cha Iboya wilayani Mbogwe mkoani Geita na hali zao zinaendelea vizuri.

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz